JE UNAFAHAMU KWAMBA KUNUKA MIGUU NI TATIZO?
➡️ Tweet
Watu wengi huwacheka watu wanaonuka miguu huku wakidhani kila mtu anayenuka Miguu ni Mchafu.
FAHAMU; Zipo sababu mbali mbali ambazo huweza Kuchangia Mtu kunuka Miguu,kama Vile;
- Ugonjwa wa Fangasi za Miguuni ambazo hushambulia maeneo mbali mbali ya mguu ikiwemo katikati ya Vidole vya Mguuni.
- Kuvaa Soksi Mbichi au Viatu ambavyo havijakauka Vizuri huleta hali ya Kunuka Miguu
- Kuvaa viatu huku miguu ikiwa michafu,mfano miguu imeshika vumbi,tope n.k
TIBA;
Tatizo la Kunuka Miguu lina tiba,kutokana na chanzo cha tatizo lako.Mfano kama tatizo ni Fangasi za Miguuni,basi utapewa dawa za kutibu Fangasi hao n.k
MAMBO YA KUEPUKA ILI USINUKE MIGUU
* Epuka Kuvaaa soksi Mbichi
* Epuka kuvaa viatu ambavyo havijakauka vizuri
* Epuka kuvaa viatu huku miguu ikiwa michafu
* Kama tatizo ni Fangasi wasiliana na wataalam wa afya kupata dawa za Fangasi
* Matumizi ya poda huweza kusaidia pia Kupunguza harufu inayotoka kwenye miguu
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!