Ticker

6/recent/ticker-posts

TATIZO LA KUPATA CHOO KIGUMU,UKOSEFU WA CHOO PAMOJA NA TIBA YAKE



🔻TATIZO LA KUPATA CHOO KIGUMU PAMOJA NA UKOSEFU WA CHOO

Watu wengi sana siku hizi hupatwa na tatizo hili la Choo Kigumu Pamoja na kukosa choo kabsa,hata kupelekea kupata Maumivu,michubuko na kutokeza kinyama sehemu za Haja kubwa ambapo kwa Kitaalam huitwa Bawasiri wakati wa Kujisaidia. Tuangalie chanzo cha Tatizo hili la Choo Kigumu,ukosefu wa choo kabsa na jinsi ya Kupata Tiba.

➡️ SABABU ZA KUTOKEA KWA TATIZO LA KUPATA CHOO KIGUMU?

Tatizo la kupata choo kigumu pamoja na ukosefu wa choo husababishwa zaidi na ulaji mbaya wa vyakula,mabadiliko ya vichocheo mwilini hasa hasa kwa Mjamzito, kuacha kula matunda na mboga na staili mbaya ya maisha ikiwa ni pamoja na kutokunywa maji ya kutosha kwa siku.


➡️ NINI KIFANYIKE ILI KUONDOA TATIZO HILI LA KUPATA CHOO KIGUMU NA KUKOSA CHOO KABSA?

Ili kuondoa tatizo kabla halijawa sugu, fanya moja miongoni mwa haya yafuatayo:

  •  Kunywa maji ya uvuguvugu asubuhi mapema, kisha tembea tembea, baada ya muda utasikia haja ya kwenda msalani. Ili usifanye haraka na upate muda wa kutosha kujiandaa kwenda kazini, amka mapema zaidi. 
  • Kula kiasi cha kutosha cha salad ya mboga mboga na juisi ya matunda halisi asubuhi kabla ya kula chochote,Kula matunda kama Mapapai,Na machungwa.
  • Kila siku kabla ya kwenda kulala, kunywa maji ya uvugu uvugu yaliyochanganywa na kijiko kimoja cha asali. Kunywa maji ya uvugu yaliyochanganywa na limau asubuhi na mapema kabla hujala kitu chochote. Kunywa castor Oil' muda mfupi kabla ya kwenda kulala.
  •  Ili kujiepusha kabisa na tatizo la ukosefu wa choo, jenga mazoea ya kunywa maji mengi, kula mboga na matunda kwa wingi kila siku na kuacha kabisa ulaji wa vyakula vilivyoondolewa virutubisho kama vile mikate myeupe, ugali wa unga mweupe, keki vyakula vyenye sukari nyingi na vyakula vingine vitamu. .

➡️ JINSI YA KUJIKINGA NA TATIZO HILI

  1. Epuka ulaji mbaya wa vyakula,
  2. pendelea kula matunda kama machungwa na Mapapai pamoja na mbogamboga au mboga za majani
  3. kunywa maji ya kutosha kwa siku angalau kuanzia lita 2.5-3 kwa Siku


                       "MWISHO"


#afyasolution #afyaclass


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!





Post a Comment

0 Comments