TATIZO LA KUTOKWA NA DAMU PUANI(NOSE-BLEEDING)

🔻TATIZO LA KUTOKWA NA DAMU PUANI(NOSE-BLEEDING)

Kutokwa damu puani ni tatizo ambalo huweza kumkumba mtu yeyote lakini huwaathiri zaidi watoto kati ya miaka 2-10 na watu wazima kati ya miaka 50 na kuendelea.


CHANZO

Mara nyingi hutokea ghafla, bila kutegemea na bila sababu maalum. Lakini kama unatokwa damu puani mara kadhaa/mara nyingi, kunaweza kuwa na sababu zifuatazo; 

.

•Hali ya joto kali

•Kuchokonoa/kupekecha pua kwa nguvu

•Hali ya baridi kali

•Jeraha katika pua kama kupigwa ngumi

•Mzio(allergy) ya madawa ambayo husababisha ukavu katika pua

•Kutumia baadhi ya madawa kama aspirin

•Maambukizi ya kipanda uso(sinusitis)

•Matatizo ya damu kutoganda vizuri mwilini •Hali tofauti za kurithi


NAMNA YA KUZUIA DAMU INAYOTOKA PUANI

1•Kuwa mtulivu: Ukihangaika hangaika unaweza kutokwa damu nyingi zaidi.

2•Kaa chini, usilale: Ili kuhakikisha kichwa chako kiko juu zaidi ya moyo wako.

3•Inamisha kichwa kidogo kwenda mbele: Hii Itazuia damu kurudi kooni. 

4•Bana pua yako: Kwa kidole gumba na cha shahada kwa dakika 5-10 ukiwa unapumulia mdomo.

5•Damu inapokata usiguseguse wala kupikicha pua kwani unaweza kutokwa damu zaidi.


UZUSHI: Ukiinamisha kichwa kurudi nyuma, damu itaingia katika ubongo.


UKWELI: Haifai kuinamisha kichwa kurudi nyuma kwani damu inaweza kurudi kooni na aidha, kungia katika njia ya hewa na kusababisha kupaliwa ama damu kuingia tumboni na kusababisha madhara mengine na kutapika.

#afyabongo #afyaclass

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!