TATIZO LA MAMA MJAMZITO KUPITISHA MDA WA KUJIFUNGUA(POSTTERM PREGNANCY),CHANZO CHAKE,DALILI NA TIBA YAKE PIA

 TATIZO LA MAMA MJAMZITO KUPITISHA MDA WA KUJIFUNGUA(POSTTERM PREGNANCY),CHANZO CHAKE,DALILI NA TIBA YAKE PIA

➡️ Ombeni Mkumbwa

Tatizo la mama kupitisha mda wa Kujifungua yaani Postterm Pregnancy linatokea pale ambapo Mimba imekaa baada ya wiki 42 za ujauzito, ambapo umevuka muda wa kawaida wa mama Kujifungua (wiki 37-40-42). Hali ya ujauzito kupitisha Mda wake huweza kuleta hatari kwa mama na mtoto, kama vile;

  •  Utapiamlo kwa mtoto(fetus)
  • Mama kupoteza maisha
  • Magonjwa yanayotokana na mtoto kunywa meconium
  • Na kuzaliwa kwa mtoto aliyekufa. Kumbuka Baada ya wiki ya 42 ya ujauzito, kondo la nyuma, ambalo humpa mtoto virutubisho na oksijeni kutoka kwa mama, huanza kuzeeka na mwisho kushindwa kufanya Kazi hiyo.


🔷 CHANZO CHA TATIZO HILI LA MAMA KUCHELEWA KUJIFUNGUA(POST TERM PREGNANCY)

Sababu za moja kwa moja zinazosababisha mwanamke kupitisha mda sahihi wa Kujifungua hazijulikani. Lakini sababu zinazochangia hali hii ni pamoja na;

- Mama kuwa na Historia ya Kuchelewa au kupitisha Mda wa Kujifungua katika Ujauzito Uliopita(History of postterm delivery from Previously Pregnancies)

- Mama kuwa na tatizo la Uzito kupita kiasi au Unene(Maternal Obesity)

- Matatizo katika Mfumo mzima wa fahamu

- Upungufu wa kiwango cha Sulphur kwenye placenta au kondo la Nyuma

- Tatizo linalohusu mtoto kuwa na shida kwenye kichwa kama vile Anecephaly

-Tarehe za matarajio(Expected date of Delivery- EDD) kwa mama Kujifungua kukosewa wakati mama akiwa hakumbuki vizuri kuhusu hedhi yake ya mwisho.  Hii huweza kusababisha mtoto kuzaliwa kabla ya Mda uliotarajiwa au kupitisha mda uliotarajiwa mama Kujifungua  

Kwahyo ni Muhimu sana mwanamke kufanyiwa Ultrasound ili kupata Majibu sahihi juu ya Tarehe hizi.

- Tafiti zinaonyesha pia mwanamke mwenye matizo katika Mzunguko wake wa hedhi kabla ya kupata mimba pamoja na Matatizo ya hormones huweza kupatwa na tatizo hili

🔻DALILI ZA MWANAMKE KUPATA TATIZO LA KUPITISHA MDA WA KUJIFUNGUA(POST TERM DELIVERY)

 ➖ Kwa sababu tatizo hili la mwanamke kupitisha mda sahihi wa kujifungua linategemea tu umri wa ujauzito, hakuna dalili za mwili zinazothibitisha uwepo wa tatizo hili.  Dalili za kawaida zinazoweza kuashiria uwepo wa hali hii ni pamoja na;

  1.  ngozi ya mwili kuwa kavu
  2. Uwepo wa mikunjo kwenye mitende ya mtoto na nyayo za miguu yao baada ya kuzaliwa
  3. Mtoto kuzaliwa na nywele nyingi kichwani, na ngozi ya kahawia, kijani kibichi, au manjano. N.k


MATIBABU

-Yapo matibabu mbali mbali kama Vile,Mama kupewa dawa ya Kuanzisha uchangu pamoja na Kuongeza uchungu ili Ajifungue kwa haraka.

- Au pia mama Kufanyiwa Upasuaji na mtoto kutolewa  Nje.

Kumbuka; Mahudhurio ya Kliniki kwa Mama Mjamzito ni muhimu sana kwani ndyo huchangia kuleta uzazi salama kwa asilimia 99% Hasa kwa mwanamke au mama ambaye hupata matatizo kipindi cha Ujauzito

KWA USHAURI ZAIDI/ELIMU/TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584

Karibu Sana..!!



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!