TATIZO LA MAUMIVU YA MGONGO KIPINDI CHA UJAUZITO
➡️ Afyabongo
#Repost @afyabongo
• • • • • •
Asilimia 75-80 ya kina mama wajawazito hupitia kipindi cha maumivu ya mgongo wakati wa ujauzito. Ni hali ya kawaida na wakati mwingine maumivu huwa makali lakini si kila mara. Maumivu haya huondoka baada ya kujifungua
Sababu kuu za maumivu haya ni
1. Mabadiliko ya kifisiolojia ambayo hupelekea misuli na ligamenti za mwili kulegea. Mabadiliko haya huchochewa na uzalishwaji wa homoni ya relaxin, ambayo hupelekea misuli na ligamenti za mgongo kulegea na kukosa uimara wake kwa muda
2. Mabadiliko ya kibayomekaniki
Katika kipindi cha kati na cha mwisho cha ujauzito, tumbo la mama huwa kubwa hivyo kupelekea uzito mkubwa mbele na kuhamisha muhimili wa uvutano wa mwili (centre of gravity). Hivyo, mzigo huelemea misuli na ligamenti za mgongo zaidi
3. Kuongezeka uzito. Ujauzito hupelekea ongezeko la takribani kilo 11 hadi 15. Uzito huu huzidia pingili za mgongo wakati wa kukaa na kupelekea mkazo
MATIBABU YA MAUMIVU YA MGONGO KIPINDI CHA UJAUZITO
1. Kuchua
2. Mazoezi laini ya kujinyoosha
3. Kuimarisha mkao
4. Kutumia maji moto kukanda
5. Msaada wa kisaikolojia unapohitajika
MUHIMU
Maumivu kipindi cha ujauzito ni kawaida na yanavumilika. Muone daktari iwapo
1. Maumivu ni makali kuliko kawaida
2. Maumivu yanasumbua kulala
3. Ganzi isioisha nyuma ya mapaja hadi miguuni.
4. Maumivu yakiendelea miezi 3-6 na zaidi baada ya ujauzito, pata matibabu
#afyabongo
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!