TATIZO LA MIMBA KUHARIBIKA ZENYEWE
➡️ Ombeni Mkumbwa
Tatizo hili limekuwa kubwa hasa katika siku za Hivi karibu,na mimba nyingi zikitoka hata kabla ya Kumaliza Miezi mitatu(3) ya mwanzoni, na wengi wao Ujauzito wa Kwanza kupata ukitoka wenyewe,Zipo sababu Nyingi ambazo husababisha Wanawake wengi kupata tatizo la Mimba Kuharibika Zenyewe- Ambapo kitaalam tunasema "The Causes of Miscariage or spontenous abortion"
NUKUUNowdays,a problem of Spontenous abortion or miscariage occurs all over the world,and There a lot of Direct and Risk Factors which contribute an Occurance of this Problem to woman
📶 SABABU ZA TATIZO LA MIMBA KUHARIBIKA ZENYEWE
Zifuatazo ni Baadhi ya Sababu Zinazochangia Kutokea kwa Tatizo hili la Mimba kuharibika au kutoka Zenyewe;
- Matatizo yanayotokana na Mfumo mzima wa Kijenetiki ambapo kitaalam hujulikana kama-Genetics Abnormalities,tatizo hili huchangia mimba kuharibika hasa hasa katika kipindi cha Miezi mitatu(3) ya Mwanzoni.
- Matatizo katika Via vya Uzazi vya Mwanamke kama Vile,Kulegea kwa shingo ya kizazi hivo kushindwa kuhimili kushikilia ujauzito hatimaye ujauzito kutoka wenyewe, Matizo kama Vile Uvimbe wa kizazi n.k
- Tatizo la Mvurugiko wa Vichocheo vyako vya Mwili ambapo kitaalam hujulikana kama Hormone Imbalance
- Uwepo wa Magonjwa mbali mbali kipindi cha Ujauzito kama vile; Ugonjwa wa kisukari, Kifafa cha Mimba,Shinikizo la Damu,Ugonjwa wa Goita na maambukizi mengine kama vile ya Rubella.
- Matumizi ya baadhi ya dawa ambazo ni hatari kipindi cha Ujauzito kama vile,matumizi ya dawa za Msongo wa mawazo mfano; paroxetine au venlafaxine
TABIA HATARISHI ZA KUPATA TATIZO LA MIMBA KUTOKA ZENYEWE
- Matumizi ya vilevi kama vile Pombe
- Uvutaji wa Sigara
- Matumizi ya vinywaji venywe Caffeine Nyingi
- Matumizi ya Dawa kiholela au Ovio bila kupewa maelekezo na wataalam wa afya
DALILI ZA MIMBA KUTOKA YENYEWE
- Kupatwa na Maumivu makali sana ya Tumbo
- Kuanza kublid au kuvuja damu wakati wa Ujauzito
- Damu nyingi kutoka ikiambatana na vipande kama maini au mabonge mabonge
VIPIMO;
Ukiwa na tatizo hilo au Dalili hizo nenda Hospital kupata vipimo mbali mbali kama Vile; ULTRASOUND,vipimo vya Mkojo,Damu n.k
MATIBABU
Yapo matibabu mbali mbali kwa Mtu mwenye tatizo hili kama Vile kusafishwa hospitalini,kupewa antibiotics kwa Ajili ya kuzuia mgonjwa asipate maambukizi mengine pamoja na Mapumziko ya Kutosha ambapo kitaalam tunaita BED-REST.
@KWA USHAURI ZAIDI/ELIMU/TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584 UPATE MSAADA,TUMA UJUMBE AU PIGA SIMU UTAHUDUMIWA POPOTE ULIPO
.
➖ SUMMARY
Katika Makala hii,tumegusia maswala mbali mbali yanayohusu tatizo la Mimba kuharibika Zenyewe kama vile;
(1) Utangulizi wa mada au makala
(2) Chanzo cha Tatizo la Mimba kuharibika zenyewe
(3) Tabia hatarishi zinazoweza kuchangia Tatizo la Mimba kuharibika zenyewe
(4) Dalili za Tatizo la Mimba kuharibika zenyewe
(5) Vipimo vya Tatizo la Mimba kuharibika zenyewe
(6) Matibabu ya Tatizo la Mimba kuharibika zenyewe
(7) Mwisho maelekezo jinsi ya kupata ushauri zaidi,elimu au Tiba kama unahitaji
afya
afyaclass
afyatips
magonjwa
magonjwa ya wanaume
magonjwa ya wanawake
magonjwa ya watoto
makala
mpya
muhimu
new
post
uzazi
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!