TATIZO LA MTOTO KUZALIWA KABLA YA WAKATI WAKE(PREMATURE BIRTH)
TATIZO LA MTOTO KUZALIWA KABLA YA WAKATI WAKE(PREMATURE BIRTH)
➡️ Ombeni Mkumbwa
Tatizo la mtoto kuzaliwa kabla ya wakati wake ambapo kwa kitaalam Hujulikana kama Premature Birth, hapa tunazungumzia mtoto kuzaliwa katika umri wa chini ya wiki 37 za ujauzito, tofauti na kawaida kuanzia wiki 37-40-42.
Watoto hawa hujulikana kama premature babies au premmies. Mwanamke huweza kupata dalili za kuzaa mapema kama vile;
- Kupata uchungu wa tumbo la uzazi ambao hufanyika mara nyingi zaidi ya kila dakika kumi
- Tatizo la kuvuja kwa majimaji kutoka ukeni
📶 VISABABISHI VYA TATIZO HILI LA MTOTO KUZALIWA KABLA YA WAKATI(PREMATURE BABIES)
Sababu ya moja kwa moja ya kuzaa kabla ya wakati haijulikani. Lakini kuna Sababu hatarishi kama vile;
- Ugonjwa wa kisukari,
- shinikizo la damu,
- kuwa na ujauzito wa watoto zaidi ya mmoja,
- kuwa mnene au mwenye uzito mdogo
- maambukizo kadhaa ukeni
- uchafuzi wa hewa pamoja na uvutaji wa tumbaku,
- Msongo wa mawazo au mafadhaiko ya kisaikolojia.
🔻MADHARA YA MTOTO KUZALIWA KABLA YA WAKATI
Watoto kuzaliwa kabla ya wakati wake yaani Premature babies wapo katika hatari kubwa ya;
➖ kupata tatizo la kupooza kwa ubongo
➖ Mtoto kuchelewa katika ukuaji wake
➖Mtoto kupata tatizo la kusikia na shida ya kuona
Mtoto Kuzaliwa kabla ya wakati ni miongoni mwa sababu zinazoongoza kusababisha vifo kwa watoto duniani. Karibu watoto milioni 15 ni premature babies katika 5% hadi 18% ya wanaojifungua wote. Katika Nchi kama Uingereza wako karibu 7.9% na huko Amerika ni karibu 12.3% ya vizazi vyote.
🔴 MAMBO YAKUZINGATIA KWA MTOTO HUYU AMBAYE KAZALIWA KABLA YA WAKATI (PREMATURE BABIES)
Yaliyomo
Ishara na dalili
1.1 Matatizo
2 Sababu za Tatizo hili
2.1 Madhara ya tatizo hili
2.2 Sababu wakati wa ujauzito
2.3 Maelekezo ya kupata huduma
KWA USHAURI ZAIDI/ELIMU/TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!