TATIZO LA VARICOSE VEINS ( KUVIMBA KWA MISHIPA YA DAMU) WAKATI WA UJA UZITO
TATIZO LA VARICOSE VEINS ( KUVIMBA KWA MISHIPA YA DAMU) WAKATI WA UJA UZITO
Varicose Veins ni tatizo linalowapata baadhi ya wanawake wajawazito. Hili ni tatizo la kuvimba na kuvunjika kwa mishipa ya damu hasa hasa kwenye maeneo ya miguu na mapaja. Pia inaweza kutoka kwenye maeneo ya njia ya haja kubwa(Hemorrhoids/Bawasiri)
Ili kujiepusha na hili tatizo ni vizuri kuongea na wamama na wadada katika ukoo au familia ili kujua kama hili tatizo liko katika familia. Mama mjamzito anabidi ajitahidi kutokustress mwili kwa kutokusimama kwa kipindi mrefu. Kuongezeka kwa msukumo wa damu wakati wa ujauzito unaweka stress kwenye mishipa, hii pamoja na kuongezeka kwa hormone aina ya Progesterone inalegeza misuli ambayo inaweza kusababisha kuvunjika kwa mishipa. Hata kama hukupata hili tatizo wakati wa ujauzito upo uwezekano wa kupata hemorrhoids au vericose veins baada ya kujifungua.
Badala ya kukaa kwenye kitu kwa muda mrefu, jaribu kukaa chini kwenye style ya kihindi yaani tailor sitting.(kama nilivyoelekeza kwenye maada ya mazoezi) Pia jaribu kuweka miguu kuelekea juu/elevated. Fanya zoezi aina la Pelvic rocking. Lala chini huku miguu ikiegemezwa juu ya kochi, kiti au kitanda huku magoti yamekunjwa. Relax katika position hii kwa dakika 10 hadi 15 halafu simama kisha piga piga miguu kwa mikono taratibu.
Fanya mazoezi ya yoga ambayo yanafanya miguu ikae kwa juu, lakini hakikisha una mtaalamu wa kukufundisha jinsi ya kufanya haya mazoezi vizuri. Kuogelea na kutembea pia ni mazoezi mazuri yanayosaidia kukupa mzunguko mzuri wa damu. Unaweza pia kupata massage ya miguu kwa dakika tano kila siku.
Usivae nguo za kubana, viatu virefu, jizuie kukunja miguu ukikaa, na kukaa kwenye kiti au gari kwa muda mrefu hivi vitu huzuia mzunguko mzuri wa damu
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!