TATIZO LA WANAWAKE KUWA NA NDEVU
TATIZO LA WANAWAKE KUWA NA NDEVU
➡️ Ndevu
• • • • • •
WANAWAKE NA NDEVU
Tatizo la mwanamke kuota ndevu na kuwa na nywele nyingi mwilini ambazo kiasili ni tabia za ukuaji wa mwanamme huwa na sababu nyingi sana.Kwa baadhi ya wanawake zinaweza kusababishwa na chembechembe asili za urithi kutoka kwa wazazi wao (ukoo wao) huku wengine zikiwa zinamaanisha uwepo wa matatizo makubwa ya kiafya kama vile mvurugiko mkubwa wa homoni,uwepo wa homoni nyingi za kiume tofauti na kiasi cha kawaida kinachovumiliwa na mwili,uzito uliozidi au hata uwepo wa Polycystic Ovarian Syndrome (PCOS),tatizo linaloathiri sehemu zinazotoa homoni za kike na kuzalisha mayai ya uzazi.
Kwa wanawake wengi,uwepo wa manyoya mengi na ndevu mwilini mwao husababishwa na PCOS au pia mvurugiko mkubwa wa homoni unaosababisha mwili uzalishe kiasi kikubwa cha homoni za kiume.Kwa wanawake hawa,hedhi zao husumbua sana na hukabiliwa na changamoto nyingi za mfumo wa uzazi ambao huleta ugumu katika kupata watoto.
Kwa wanawake walio na ndevu au manyoya mengi na bado hawajabahatika kupata watoto watafute msaada wa matibabu haraka ili wasaidiwe,kwao tatizo hili linaweza lisiwe la kurithi na linaweza kuwa dalili muhimu ya uwepo wa matatizo kwenye miili yao.Kwa wanawake walio na watoto tayari na wanazo ndevu au manyoya mengi wanaweza pia kutafuta msaada wa matibabu,japo sababu kubwa kwao inaweza kuwa ni kurithi na wanaweza wasiwe na shida yoyote. CR:@afyadarasa
#afyadarasa
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!