UGONJWA WA GOITA,MAANA YAKE,CHANZO,DALILI NA TIBA YAKE

FAHAMU UGONJWA WA GOITA


Goita (Goiter) ni hali ya kuvimba kwa tezi ya thyroid. Uvimbe huu hautokani na saratani (goita si saratani). Tezi ya thyroid ipo sehemu ya mbele ya shingo. Kazi kuu za tezi ya thyroid ni kuzalisha homoni mbalimbali ambazo husaidia mwili kuthibiti na kufanya kazi zake mbalimbali.


VIHATARISHI VYA GOITA

 

Kuna baadhi ya mambo yanayohusiana na kurithi yanayoweza kusababisha mtu kupata goita. Vihatarishi hivi ni pamoja na:


1. Kuwa na umri kuanzia miaka 40 na kuendelea


2. Historia ya ugonjwa wa goita miongoni mwa wanafamilia


3. Hali ya kuwa mwanamke


4. Na, kutopata iodine ya kutosha katika lishe. Iodine ni madini muhimu yanayohitajika katika utengenezaji wa homoni mbalimbali zinazozalishwa na tezi ya thyroid. Watu wanaoishi kwenye maeneo mbali kutoka pwani ya bahari au yaliyo katika nyanda za juu kutoka usawa wa bahari kama vile mikoa ya Mbeya, Iringa na Rukwa wapo katika hatari ya kupata goita kwa vile hawapati madini ya kutosha ya Iodine katika chakula chao.


•Soma: Ugonjwa wa Mgongo Wazi kwa Watoto,chanzo,Dalili na Tiba yake


DALILI ZA GOITA 


Dalili kuu ya goita ni kuvimba au kuongezeka ukubwa kwa tezi ya thyroid. Ukubwa wa tezi unaweza kuwa kijiuvimbe kidogo katika tezi au uvimbe mkubwa kama nundu sehemu ya mbele ya shingo. Kuvimba kwa tezi ya thyroid kunaweza kusababisha mgandamizo katika njia ya hewa na mrija wa chakula, hali ambayo inaweza kusababisha:


1. Shida katika kupumua


2. Kikohozi


3. Sauti kuwa ya mikwaruzo


4. Shida wakati wa kumeza chakula


5. Wakati mwingine, mishipa ya damu ya shingoni inaweza kuvimba pia na kusababisha mtu kujihisi kizunguzungu pindi anapoinua mikono juu


MADHARA YA GOITA 


1. Shida wakati wa kumeza au kupumua


2. Kiwango cha chini cha homoni za thyroid (Hypothyroidism)


3. Kiwango cha juu cha homoni za thyroid (Hyperthyroidism)


4. Saratani ya tezi ya thyroid (thyroid cancer)


5. Goita yenye vivimbe inayozalisha homoni kwa wingi (toxic nodular goiter)


#afyabongo #drtareeq #afyaclass


•Soma: Ugonjwa wa Mgongo Wazi kwa Watoto,chanzo,Dalili na Tiba yake


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!