Ufahamu ugonjwa wa Malaria
Malaria ni ugonjwa unaosababishwa na vimelea vinavyojulikana kama Plasmodium.Vimelea hivi huenezwa na mbu jike aina ya anofelesi (anopheles). Lakini watu wengi huelewa kwamba malaria husababishwa na mbu. Mbu huyu husaidia katika usambazaji tuu wa vimelea husika.
Aina ya vimelea ambavyo humdhuru binadamu kati ya vimelea vingi vya Plasmodium ni:
• Plasmodium Vivax
• Plasmodium Falciparum
• Plasmodium Malariae
• Plasmodium Oval
Plasmodium Vivax: Vimelea hivi havina madhara makubwa ingawa vimesambaa sana kuliko vile vya Plasmodium Falciparum.
Plasmodium Falciparum: husababisha vifo vingi na kwa haraka zaidi.
Vimelea vingine kama Plasmodium Malariae na Plasmodium Oval husababisha pia malaria lakini sio kwa ukali na yenye uharibifu kama vile vya Plasmodium Falciparum. Ukurasa huu umejizatiti zaidi kuzungumzia malaria inayosababishwa na Plasmodium Falciparum, kwani ndio inayotushambulia zaidi ukanda huu wa Afrika Mashariki. (Cc @afyatrack.com)
DALILI ZA UGONJWA WA MALARIA
Mwaka huu tunakwenda na kauli mbiu kuwa “KIWANGO SIFURI CHA MALARIA KINAANZA NA MIMI”
Chukua Hatua
Jinsi ya kuzuia maambukizi ya Malaria
1. Kuzuia mazalia ya mbu
Fyeka vichaka na ondoa madimbwi ya maji katika maeneo yanayokuzunguka.
2. Kuzuia kung’atwa na mbu kwa:
i. Matumizi ya vyandarua vyenye dawa ya kuua mbu
ii. Matumizi ya dawa za kupulizia za kuua mbu majumbani
iii. Matumizi ya dawa za kupaka za kuua mmbu
3. Dawa za kuzuia malaria kwa kina mama wajawazito (IPT)
Sulfadoxine Pyrimethamine (SP) hutolewa kwa kina mama katika wiki ya 20 na wiki ya 36 ya ujauzito.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!