UGONJWA WA TYPHOID(HOMA YA MATUMBO

TYPHOID NI NINI?

Ni ugonjwa wa homa ya matumbo unaosababishwa na bakteria ajulikanae kama, Salmonella typhi. Homa hii huhusisha homa inayopanda juu taratibu mpaka kufikia joto la 40⁰C


HUAMBUKIZWAJE?

Bakteria hawa wa Salmonella typhi husambazwa kupitia kula vyakula/maji yaliyochafuliwa/kuingiwa na kinyesi/mkojo wa mgonjwa wa typhoid au carrier(mtu anayebeba ugonjwa anaweza kuambukiza wengine ila yeye haugui)

.

DALILI 

Typhoid huhusisha homa inayopanda taratibu mpaka kuweza kufikia joto la 40⁰C, kutokwa jasho jingi, maambukizi katika tumbo na utumbo(gastroenteritis) na kuhara kawaida ama damu


Mara chache mgonjwa anaweza kuwa na upele wa pink kwenye ngozi


Muda wa Utungishwaji(incubation period) wa typhoid hutofautiana kulingana na dozi ya maambukizi (yaani wadudu kiasi gani waliokuingia) na kipindi hiki huwa kati ya siku 10-20


Typhoid isiyotibiwa dalili zake hugawanyika katika wiki kama ifuatavyo


1. DALILI KATIKA WIKI YA KWANZA

Huwa hazieleweki zikijumuisha kichwa kuuma, uchovu, homa kali inayopanda, kukosa choo, kikohozi kikavu na mapigo ya moyo kwenda taratibu .

.

2. DALILI KATIKA WIKI YA PILI

Kama bado hujatibiwa, joto la mwili huzidi kupanda na zaidi ya nusu ya wagonjwa huanza kuharisha. Mgonjwa huonekana dhoofu na tumbo kuvimba upande wa kongosho(splenomegally), pia Mapigo ya moyo huwa hafifu .

.

3. DALILI KATIKA WIKI YA TATU

Mgonjwa huzidi kuwa hoi na kuanza kuchanganyikiwa, kutotulia na tatizo la akili la kusikia mambo yasiyokuwepo(hallucinations). Kuharisha uharo wenye harufu mbaya wenye rangi ya kijani/njano(kama supu ya njegere)


Mapigo ya moyo huwa legelege(feeble) na ya kasi(rapid), kupumua kwa kasi


KIFO huweza kutokea katika wiki hii kutokana na usumu kwenye damu(toxemia), maambukizi katika misuli ya moyo(myocarditis), utumbo kuvuja damu/kutoboka. Pia maambukizi ya ubongo(encephalitis) 

(NA afyabongo)

#afyaclass 

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!