UJUE UGONJWA WA GOUT,CHANZO CHAKE,VIHATARISHI,DALILI NA MATIBABU YAKE
UJUE UGONJWA WA GOUT,CHANZO CHAKE,VIHATARISHI,DALILI NA MATIBABU YAKE
• • • • • •
Gauti inaweza kutokea ghafla (acute gout) au ikawa sugu (chronic gout). Gauti inayotokea ghafla huwa na maumivu makali na mara nyingi huathiri jointi moja tu wakati gauti sugu inaweza kuathiri jointi zaidi ya moja na huambatana na hali ya kujirudia ya maumivu na uvimbe kwenye jointi
📚VISABABISHI
Gauti husababishwa na kuwepo kwa kiwango kikubwa kuliko kawaida cha uric acid katika damu. Hali hutokea iwapo mwili wa mgonjwa unatengeneza uric acid nyingi kuliko kawaida au unashindwa kutoa uric acid mwilini kama inavyotakiwa.
Ongezeko hili husababisha mrundikano wa uric acid katika maji maji yanayozunguka jointi yanayoitwa synovial fluid na hatimaye kutengeneza vijiwe vidogo vidogo vya tindikali ya urea yaani uric acid crystals ambavyo husababisha jointi kuvimba na hatimaye kuathirika
📚VIHATARISHI (risk factors)
Ugonjwa wa gauti hutokea kuwapata baadhi ya watu walio katika familia moja. Wanaume huathiriwa zaidi kuliko wanawake ingawa wanawake waliokoma kupata hedhi huathiriwa zaidi kuliko wale wanaoendelea kupata hedhi.
Aidha unywaji pombe unachangia kwa kiasi kikubwa kuwepo kwa ugonjwa huu pamoja na matumizi ya baadhi ya madawa kama vile dawa za kutoa maji mwilini ambazo kwa ujumla husababisha ongezeko la kiwango cha uric acid katika damu.
Vihatarishi vingine vya gauti ni pamoja na kuwa na ugonjwa wa kisukari, magonjwa ya figo, unene uliopitiliza, ugonjwa wa sickle cell anemia au aina nyingine za upungufu wa damu, pamoja na saratani ya damu (leukemia).
Hali kadhalika, gauti inaweza kusababishwa na matumizi ya dawa ambazo utendaji wake kazi huingiliana na utoaji wa uric acid mwilini.
📚DALILI
1. Dalili za gauti kwa kawaida uhusisha jointi moja au joint chache. Jointi zinazoathiriwa zaidi ni pamoja na kidole kikubwa ha mguuni, magoti, au kiwiko cha mguu.
2. Wagonjwa huwa na maumivu yanayoanza kwa ghafla hususani nyakati za usiku. Maumivu makali kama kitu kinachokata, kupwita au mifupa inayosagana.
3. Jointi hubadilika na kuwa na joto, kuvimba na kuwa na nyekundu (hujionesha zaidi kwa watu wenye ngozi nyeupe).
4. Shambulio linaweza kudumu kwa siku kadhaa kabla mgonjwa hajapata nafuu.
5. Pia mgonjwa anaweza kupata homa
#afyabongo #afyacheck_
CR:@afyabongo
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!