UVIMBE KWENYE KIZAZI(FIBROIDS)

  UVIMBE KWENYE KIZAZI(FIBROIDS),CHANZO CHAKE,DALILI ZAKE,MADHARA YAKE NA TIBA YAKE






➡️ Ombeni Mkumbwa


🔺SUMMARY

Katika Makala hii,tutajadili kwa kina,hasa hasa katika Vipengele vifuatavyo;

➖ Maana ya Uvimbe kwenye kizazi

➖ Chanzo au visababishi vya Uvimbe kwenye kizazi

➖ Watu ambao wapo kwenye hatari ya Kupata Tatizo hili la Uvimbe wa Kizazi

➖ Dalili au viashiria vya kuwepo kwa Uvimbe kwenye kizazi

➖ Madhara ya Kupata Uvimbe kwenye kizazi

➖ Tiba sahihi ya Tatizo hili la Uvimbe kwenye Kizazi

➖ Maelekezo ya Kupata ushauri,Elimu au Tiba popote Ulipo


Utangulizi;

🔷 UVIMBE KWENYE KIZAZI NI NINI?

Uvimbe kwenye Kizazi ambapo kwa Kitaalam Hujulikana kama "FIBROIDS"- ni aiana ya Uvimbe ambao hutokea katika kuta za ndani za Mji wa mimba(Kizazi) au Uterus,au katikati ya kuta za Mji wa mimba,hivo kuleta madhara mengi. Kuta hizo za Mji wa mimba au Uterus zimegawanyika katika Maeneo au sehemu kuu Tatu.

 

       (i) Ukuta wa Ndani kabsa-ambao                        hujulikana kitaalam kama                   Endometrium
       (ii) Ukuta wa katikati-ambao kitaalam hujilikana kama Myometrium
       (iii) Na ukuta wa Nje ya Uzazi-ambao kitaalam hujulikana kama Serosa

Sasa basi Kutokana na Mgawanyiko huo wa kuta za Mji wa mimba(Uterus), hapo ndipo aina za Uvimbe wa Kizazi au Fibroids zikatokea.

🔻Kuna aina kuu Tatu za Uvimbe wa Kizazi(FIBROIDS)

  • Kuna Submucosal Fibroids- ambayo hii ni Uvimbe wa Kizazi lakini unatokea sehemu ya Ndani ya Kizazi
  • Intramural fibroids- hii ni aina ya Uvimbe wa Kizazi unaotokea sehemu ya katikati ya Kizazi
  • Subserosal Fibroids-aina hii ya Uvimbe wa Kizazi hutokea sehemu ya Nje ya Kizazi

🔴Kumbuka; Uvimbe kwenye kizazi Huweza kutokea katika maeneo mbali mbali ya Kizazi Mfano;  

Kuna Uvimbe wa vifuko vya mayai yaani kitaalam Hujulikana kama Ovarian Cysts

Kuna uvimbe kwenye kuta za Mji wa Uzazi kama nilivyoelezea hapo mwanzoni

 Kuna uvimbe unaoweza kutokea kwenye Mirija ya Uzazi,na kuleta tatizo la kuziba kwa Mirija ya Uzazi 

CHANZO CHA UVIMBE KWENYE KIZAZI AU FIBROIDS

Hakuna sababu ya Moja kwa moja ya mtu kupata Tatizo hili la Uvimbe wa kizazi,Japo kuna vitu ambavyo huweza kuchangia mtu kupata Uvimbe kwenye Kizazi, Kama vile;
  1. Matumizi ya dawa ambazo zina vichocheo vingi ndani yake,hasa vile vinavyohusika na Ukuaji wa seli hai za mwili kama vile progesterone,estrogen,n.k
  2. Tatizo la Unene pamoja na Uzito kupita kiasi
  3. Matumizi ya Njia mbalimbali za Uzazi wa Mpango
  4. Unywaji wa Pombe na matumizi ya vyakula vyenye sukari nyingi pamoja na Proteins

KUNDI LA WATU AMBAO WAPO KATIKA HATARI YA KUPATA TATIZO LA UVIMBE WA KIZAZI

  • Umri wa kuanzia kubalehe au kuvunja Ungo mpaka ukomo wa hedhi
  • Mwanamke ambaye hajawahi kupata mtoto hadi kufikia umri mkubwa
  • Watu wanene na wenye Uzito Kupita Kiasi
  • Wanawake waliowahi kuingia hedhi
  • Kuwa na historia ya Tatizo la Uvimbe wa Kizazi katika Familia yenu

DALILI ZA TATIZO LA UVIMBE WA KIZAZI

Hizi hapa ni baadhi ya Dalili ambazo huweza Kujitokeza kwa mtu mwenye tatizo la Uvimbe kwenye kizazi;

1️⃣ Kutokwa na Damu ya Hedhi au kupata period katikati ya mwezi

2️⃣ Maumivu makali ya Tumbo hasa wakati wa Hedhi,kwani tumbo la Uzazi hujaribu kuusuka Ule Uvimbe kutoka Nje,Kitendo hiki huleta maumivu makali

3️⃣ Kupata maumivu makali ya Tumbo na Kiuno wakati wa Tendo la Ndoa

4️⃣ Kutokwa na Uchafu mwingi ukeni na wakati mwingine huambatana na harufu kali sehemu za Siri,hasa hasa kama uvimbe umeziba mirija ya Uzazi(fallopian Tubes)

5️⃣ Kutokwa na Damu wakati wa tendo la Ndoa, pamoja na mvurugiko wa Mpangilio wa siku za Hedhi

🔻Uvimbe ukiwa Mkubwa sana huweza kuleta dalili kama hizi;

- Kukojoa mara kwa mara,kwani nafasi kubwa ya uvimbe husababisha mgandamizo wa kibofu cha Mkojo

- Mkojo kubakia kwenye kibofu mara baada ya kukojoa

 - Kupata Choo kigumu sana,hata kukuletea maumivu makali sehemu ya Haja kubwa pamoja na Michubuko

MADHARA YA KUWA NA TATIZO LA UVIMBE WA KIZAZI 

  1. Maumivu makali wakati wa Hedhi na wakati wa Tendo la Ndoa
  2. Kutokwa na Uchafu mwingi ukeni na wenye harufu mbaya
  3. kutolewa kizazi chote wakati wa matibabu kama uvimbe umeathiri sehemu kubwa ya Kizazi
  4. Tatizo la kushindwa kubeba Ujauzito
  5. Mvurugiko wa siku za Hedhi,ikiwemo kupata hedhi katikati ya mwezi

MATIBABU YA UVIMBE WA KIZAZI 

Kama una tatizo la Uvimbe kwenye kizazi Wasiliana na wataalam wa afya, Kuna dawa za kusaidia Uvimbe huu kuisha, Lakini pia endapo tatizo litashindikana,Njia ya mwisho kabsa ni kufanyiwa Upasuaji na Uvimbe huo kutolewa kabsa.

KWA USHAURI ZAIDI/ELIMU/TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584




2 Comments

  1. Asante Sana Dr kwa mafundisho haya hakina Sasa nimeanza kuelewa mwili wangu

    ReplyDelete

WEKA COMMENT HAPA..!!!