UVIMBE KWENYE MIDOMO YA UKE

 TATIZO LA KUWA NA UVIMBE KWENYE MASHAVU AU MIDOMO YA UKE

Tezi za Bartholin huwa ki kawaida zinapatikana katika pande za mashavu/midomo ya uke. Huwa ni ndogo mno na hufanya kazi ya kutengeneza uteute/majimaji ili kufanya uke kuwa na unyevunyevu na kuepusha ukavu


Uteute huu husambazwa ukeni kupitia vimirija vidogo (ducts). Inapotokea kuna kizuizi (blockage), uteute huu hujaa na kusababisha tezi kuvimba, na ndio huitwa BARTHOLIN CYST


CHANZO

Wataalamu mpaka sasa hawana jibu la uhakika kwa nini kizuizi hutokea na kusababisha uvimbe. Lakini huhusishwa na maambukizi ya Magonjwa ya Zinaa kama Kisonono na Pangusa


NANI YUPO KATIKA HATARI?

Wanawake kati ya umri wa miaka 20 mpaka 30, japo huweza kutokea pia katika umri mwingine. Uwezekano wa kupata tatizo hupungua kadri umri unavyo ongezeka. Wanawake 2 kati ya 10 hupatwa na tatizo hili


DALILI

Unaweza usiwe na dalili zozote mpaka uvimbe unapokuwa mkubwa zaidi ama unapopata maambukizi (infection)ya bakteria •Maumivu makali katika uvimbe

•Maumivu katika tendo la ndoa

•Maumivu wakati wa kutembea

•Uvimbe ukiwa mkubwa hushusha zaidi shavu la uke katika pande husika

•Homa (kutokana na maambukizi)

•Kutokwa na uchafu (discharge)


Soma: Tatizo la uke Kujamba,chanzo na Tiba yake


MATIBABU

1•Kama una umri chini ya miaka 40 na uvimbe haukupi shida, Fanya "Sitz Bath"- Weka maji ya vuguvugu katika beseni kisha kalia maji kwa dakika 15-20, hakikisha maji yanafunika eneo lote la uke. Fanya hivi mara 3 kila siku kwa siku 4. Uvimbe utatoweka wote na utarudi kama zamani

.

.

2•Kama uvimbe unaleta shida, daktari ataamua kati ya Tiba zifuatazo

》Upasuaji na kutumbua (Surgical Drainage)

》Marsupialization (Kutumbua na kushona nje ndani) hii kuzuia tatizo kujirudiarudia

》Upasuaji wa kuondoa tezi yote •Kama Vipimo vitaonesha una maambukizi ya Magonjwa ya Zinaa utapata pia Tiba husika

(NA @afyabongo)

#Afyaclass


Soma: Tatizo la uke Kujamba,chanzo na Tiba yake


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!