AFYA BORA KWA MTOTO
Afya bora kwa mtoto ipo mikononi mwako.Kuna mambo muhimu lazima uyafanye kwa mtoto kuanzia tu pale anapozaliwa.
.
Jambo la kwanza kabsa ni kuhakikisha unaanza kumnyonyesha ndani ya lisaa la kwanza mara tu baada ya kujifungua
.
Unyonyeshaji huo unaenda mpaka miez sita pasipo kumchanganyia kitu kingine chochote,Baada ya miezi sita anza kumchanganyia mtoto vyakula pamoja na maziwa ya mama
.
Hiyo nayo inaenda mpaka mtoto akifika miaka miwili,hapo utakuwa umezingatia unyonyeshaji bora kwa mtoto wako,na kumbuka maziwa ya mama ndo kinga kubwa kwa mtoto dhidi ya magonjwa
.
Jambo lingine ni kuhakikisha mtoto anapata chanjo zote muhimu kuanzia anapozaliwa mpaka anapofikisha umri wa miaka mitano
.
Usafi kwa mtoto ni jambo la muhimu kwa mtoto pia, na kuzingatia swala la kutokuweka kitu chochote kwenye kitovu cha mtoto mpaka kidongoke chenyewe
.
Pia zingatia dalili zote za hatari kwa mtoto ili uzionapo tu uhakikishe mtoto anapata msaada wa kitaam,mfano mtoto kugeuka rangi na kuwa manjano,mtoto kupatwa na degedege,mtoto kutokunyonya kabsa,n.k
#mtoto
#afya
#ombenimkumbwa
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!