AINA 6 ZA UTE (RANGI,MUONEKANO NA MAANA ZAKE)

UTE

• • • • • •

AINA 6 ZA  UTE (RANGI,MUONEKANO NA  MAANA ZAKE)


Utoaji wa ute kutoka kwenye uke huwa na maana kubwa sana katika kusafisha bakteria na seli zilizokufa.Kwa asili yake,uke ni kiungo kilicho na utaratibu wake wa kujisafisha tofauti na viungo vingine vya mwili hivyo huwa unahitaji msaada mdogo tu wa usafi kutoka nje.Hulenga  kuleta uwiano sawa wa usafi wa ndani pamoja na homoni&kemikali zilizo ndani ya mwili


Ikitokea uwiano huu umeharibiwa kwa namna yoyote (dawa,kisukari,dawa za kuzuia mimba,sabuni zenye harufu&lotions,vyakula&msongo wa mawazo au kutokana na uwepo wa magonjwa) ndipo huwa tunapata rangi tofauti kama nilivyoeleza hapa chini


1)UTE MZITO UKIWA MWEUPE(HAUNA RANGI)

Inamaanisha upo kwenye siku zako za hatari kabisa katika mzunguko wako.Kama unahaja ya kupata mtoto basi kifanyie kazi kipindi hiki  na ikiwa hauna mpango huo basi usithubutu kukutana na mwanaume bila kutumia kinga


2)UTE MWEPESI UKIWA MWEUPE(HAUNA RANGI)

Mara nyingi huwa hauashirii tatizo lolota la afya.Hutokea siku chache kabla hujaanza hedhi


3)KIJANI AU URUJUANI

Huashiria kuwa umeshambuliwa na bakteria (bacterial vaginosis au trichomonas).Huambatana na miwasho hivyo tafuta msaada wa tiba


4)UTE KAMA UNGA MKAVU/MBICHI

Unaweza ukawa unaonekana kama  unga mbichi au mkavu usiolowanisha sana nguo ya ndani,bali unajikusanya tu sehemu moja.Ni ishara ya yeast infection hivyo pata msaada wa matibabu kwani pia hubatana na miwasho


5)NJANO

Ni ishara ya maambukizi ya magonjwa hasa ya ngono (kaswende au kisonono).Mara nyingi huambatana na miwasho,maumivu,kutokwa na usaha,maumivu wakati wa kukojoa pamoja na maumivu ya nyonga.Tafuta msaada wa tiba


6)RANGI YA UDONGO/DAMU CHAFU

Ni ishara ya kuwa mzunguko wako hauko sawa.Ukiwa katikati ya mzunguko na ukatokewa na hali hii inabidi ufanye uchunguzi.Mara nyingi hali hii hutokea kwa wale wanaoanza kutumia dawa za kuzuia mimba/kupanga uzazi.Mbali na jambo hili,hali hii hujidhihirisha pia kwa watu wanaougua au walio katika hatari ya kukumbwa na saratani ya shingo ya mlango wa uzazi  au kama ujauzito umetungwa nje ya mfuko wa uzazi (ectopic pregnancy)





0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!