AINA YA MAUMIVU YA KICHWA AMBAYO NI HATARI KWA AFYA YAKO

KICHWA KUUMA

• • • • • •

AINA YA MAUMIVU YA KICHWA AMBAYO NI HATARI KWA AFYA YAKO


Sio kila Maumivu ya kichwa ni yakawaida na yakupuuzia kama watu wengi wanavyodhani. Ipo aina ya maumivu ya kichwa ambayo huhitaji msaada wa haraka wa kiafya kwani Ishara yake ni mbaya.


Kuumwa na kichwa ni swala la kawaida kwa kila binadamu,lakini leo nakufundisha ujue kutofautisha kati ya maumivu ya kawaida ya kichwa na maumivu ambayo ni hatari sana kwa afya yako.


AINA YA MAUMIVU YA KICHWA AMBAYO NI HATARI KWAKO


  • Kuumwa na kichwa sana kunakoenda sambamba na uwepo wa homa kali kwa wakati Mmoja
  • Kuumwa na kichwa sana kunakoenda sambamba na kuwepo kwa hali ya kupoteza fahamu au kumbukumbu
  • Kuumwa na kichwa sana kunakoenda sambamba na hali ya kutingishwa kwa Mwili
  • Kuumwa na kichwa sana kinachogonga mithili ya Mtu anagonga na Nyundo
  • Kuumwa na kichwa sana kunakoenda sambamba na shida ya shingo Mfano kukakamaa kwa shingo n.k
  • Kuumwa na kichwa sana kunakoenda sambamba na hali ya kuchanganyikiwa kabsa


Ukihis aina hii ya Maumivu ya kichwa, Fanya haraka sana kuonana na wataalam wa afya kwa Ajili ya matibabu sahihi ya Shida yako.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584





0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!