PROTEIN
• • • • • •
Watu wanaokula chakula kingi asubuhi kuliko usiku,huwa na nafasi nzuri ya kupunguza uzito wa mwili.Wale wanaokula kiasi kikubwa cha chakula kabla ya kulala huongeza nafasi ya kupata obesity (uzito uliozidi).Kiafya,inashauriwa ule chakula kingi asubuhi kuliko usiku.
Pia,ni vyema kupata mlo wa usiku saa 2 hadi 3 kabla ya kwenda kitandani kulala.Kula chakula hapohapo kisha unapumzika ni miongoni mwa sababu zinazopelekea watu kupata ongezeko la uzito pasipo kuelewa chanzo chake ni nini,ni lazima kuruhusu taratibu za awali za mmeng'enyo wa chakula zifanyike kabla hujaamua kupumzika
-
Unapoanza siku yako kwa kula chakula chenye utajiri mwingi wa protini husaidia kukufanya ujisikie umeshiba kwa muda mrefu.Hii itandoa uhitaji wa kula mara kwa mara hasa nyakati za mchana.Mfano wa vyakula hivyo ni maziwa,nyama ya kuku,samaki,mayai,dairy products kama yoghurt na cheese,karanga,korosho,maharage,maharagwe,broccoli,parachichi,ndizi,maboga (hasa mbegu zake) na supu (ng'ombe,mbuzi n.k)
Via sainiyaafya
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!