ATHARI ZA JOTO KALI KIAFYA

JOTO KALI

• • • • • •

Kawaida kipindi cha miezi ya Oktoba- Machi kila mwaka jua la utosi linakuwa katika maeneo ya kizio cha kusini mwa dunia.

Tanzania ikiwa ni moja ya nchi zilizopo katika kizio cha kusini, huwa na joto kali katika maeneo mengi ikilinganishwa na miezi mingine. 


Joto kali husababisha mwili hupoteza maji mengi pamoja na madini chumvi. 


Iwapo mwili ukiendelea kupandisha joto bila kupoa unaweza pata  madhara mbalimbali

1. Mwili kuelemewa na joto

2. Misuli kukakama

3. Kiharusi cha joto kali 


Wazee, Watoto, Watu wenye magonjwa ya kudumu kama upumuaji na moyo, Watu wenye homa kali kutokana na magonjwa kama malaria, Watu wanaotumia pombe kupita kiasi na Watu wenye unene uliokithri. 

Ni makundi ya watu ambao hupata madhara ya joto kali kwa urahisi zaidi


Joto kali huweza kusababisha Tatizo la Misuli kukakamaa Kipindi cha joto kali. Tatizo hili hutokana na mwili kupoteza maji mengi na madini chumvi muhimu kama sodium. Inapotokea hali hii kunywa maji mengi yenye hasa yenye chumvi kiasi 


Mwili ukilemewa na joto kali bila kupata tiba mtu huweza pata Kiharusi cha joto kali


DALILI ZA KIHARUSI CHA JOTO KALI

- Moyo kwenda mbio na kupumua haraka,

- ngozi kuvilia

- Ngozi kuwa kavu au kunanata

- Kuchanganyikiwa

- Kupoteza fahamu au kupata degedege. 


(Waliopita jeshi wanaelewa)


KIPINDI HIKI CHA JOTO 

➡️Kunywa maji ya kutosha

➡️Vaa nguo nyepesi hasa zisizo na rangi nyeusi

➡️Usiache Watoto ndani ya gari lililopaki


(đź“ťNormanJonasMD)

.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!





0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!