ATHARI ZA ULAJI WA MAYAI MABICHI

Ulaji mwingi (uliopitiliza) wa mayai YASIYOCHEMSHWA/MABICHI kunaweza kupelekea kutokea kwa matatizo kama vile kunyonyoka kwa nywele,kupauka kwa ngozi,kuvunjika ama kujikunja kwa kucha pamoja na msongo wa mawazo.Kwa watoto inaweza kupelekea wawe na afya dhaifu pamoja na kupungua uzito wa mwili.

-

Mayai haya huwa na kiasi kikubwa cha protini aina ya AVIDIN ambayo huwa na uwezo wa kuungana na hivyo kuzuia ufanyaji kazi wa protini nyingine muhimu sana ambayo ni BIOTIN.Jambo hili linapotokea,madhara tajwa huko juu hudhihirika

-

Mayai mabichi huwa pia na kiasi kikubwa cha bakteria jamii ya Salmonella ambao ni hatari kwa afya. Bakteria hawa wanaweza kusababisha tatizo la “sumu ya chakula” ama food poisoning kwa mhusika hiyo kusababisha kuharisha,kutapika,homa kali,maumivu ya kichwa,maumivu makali ya tumbo pamoja na upotevu wa maji mengi mwilini. Hali inaweza kuwa mbaya zaidi kwa mama mjamzito kwa kusababisha ajifungue kabla ya wakati au hata kuharibika kwa ujauzito

-

Unapokuwa unapika ama kuchemsha mayai yako hakikisha yanaiva vizuri ili kuiharibu avidin-kuifanya ipoteze uwezo wa kuathiri biotin pamoja na kuwaharibu bakteria wa Salmonella. Wastani wa dakika 15-20 hutosha kabisa kuivisha mayai hasa yakiwa kwenye vimiminika vilivyochemka.cc.afyainfo


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!