UZAZI
• • • • • •
BAADA YA KUJIFUNGUA.
Mwanamke aliyetoka kujifungua anahitaji kipindi maalumu kwa ajili ya kupona na kurejesha mwili wake katika hali ya kawaida.
Baada ya kujifungua tegemea;
1. Mji wa mimba (uterus) kurejea katika ukubwa wake wa kawaida baada ya wiki 2 mpka 6 baada ya kujifungua. Hii itaambatana na maumivu ya tumbo kama yale yanayotokea wakati wa hedhi. Lakini hii haimaanishi tumbo litapungua haraka na pia michirizi nayo itahitaji muda mwingi zaidi kupotea.
2. Tegemea kutokwa na damu nzito ndani ya siku mbili au tatu baada ya kujifungua. Damu hii itaenda ikipungua taratibu pia ukibadilisha kutoka kuwa nyekundu sana mpaka kuwa rangi ya kahawia. Bado unaweza kuona marine ya damu ya mpaka wiki ya sita baada ya kujifungua.
3. Maumivu ya kukata katika uke. Hii hutokea kama uliongezewa njia, au ulichanika msamba au hata kama haikutokea kitu kama hiko.
4. Maumivu wakati wa kukojoa na shida ya kukojoa.
Prepared by Dr Sam
“JIFUNZE na Chukua Hatua Juu Ya Afya Yako”.
.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!