CHAKULA NA HEDHI
• • • • • •
CHAKULA KISICHOFAA WAKATI WA HEDHI.
Hedhi ni kipindi maalumu katika mzunguko wa siku za mwanamke mwenye umri wa kuzaa. Hedhi bora ni dalili ya afya njema ya uzazi. Kabla sijakueleza vitu vya kutotumia wakati wa hedhi ni vema nikakufahamisha sifa za hedhi iliyobora.
Kama wewe ni mwanamke na utaona kuna kitu hakipo sawa katika hedhi yako ni vema uwahi kupata msaada ili kuboresha afya yako ya uzazi.
• Hedhi ilibora hupatika mara moja kwa mwezi yaani kama mzunguko wako ni siku 28 basi hedhi yako itapatikana kila baada siku 28. Kama hedhi haitabiriki ujue kuna shida ambayo unapaswa kuitatua ili upate hedhi iliyobora.
• Hedhi iliyobora haiambatani na maumivu makali, kwa kawaida maumivu ya hedhi hayapaswi kumfanya mwanamke kuacha kufanya shughuli zake za kawaida. Kama unapata maumivu makali sana wakati wa hedhi basi ujue hedhi yako ina shida.
• Hedhi iliyobora hupatikana siku tatu mpaka saba. Katika mzunguko wa mwezi siku za hedhi zinapaswa kuwa tatu mpka saba. Chini au zaidi ya hapo ni ishara ya hatari katika afya yako ya uzazi.
• Hedhi iliyobora damu yake si nzito sana yenye mabonge mabonge au nyepesi sana kama maji yenye rangi ya damu. Hii si dalili njema kwa mwanamke kupata aina hii ya hedhi.
• Kiwango cha damu ya hedhi iliyobora huwa ni cha kawaida si damu nyingi sana inayopelekea mwanamke kubadili (pads) mara nyingi kwa siku, au damu chache sana vitone tu vichache vya damu kila mwezi.
Sasa tuangalie vitu ambavyo mwanamke hapaswi kupendelea kutumia anapokua kwenye siku zake za hedhi:
• Vinywaji vyenye caffeine (kahawa, chai)
• Pombe kwa aina zake
• Vinywaji vyenye sukari nyingi
• Vyakula vyenye mafuta mengi.
• Kufanya mazoezi makali sana
Ulaji wa vyakula hivi kwa kiwango kikubwa husababisha ongezeko la prostaglandin(kichocheo kinachoshusha kuta za uzazi kama mimba haijatungwa na kuandaa eneo la mimba kwa utungishwaji mwingine wa mimba). Kuongezeka kwa vichocheo hivi husababisha kukaza na kusinyaa kwa misuli ya mfuko wa kizazi kwa kiasi kikubwa sana na husababisha maumivu makali wakati wa hedhi.
Mwanamke awapo kwenye hedhi anashauriwa kula mbogamboga na matunda yasiyo na sukari pamoja na nyama nyekundu ili kumuongezea madini ya chuma.
by Dr Sam,
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!