CHANZO CHA MAUMIVU YA TUMBO MARA KWA MARA

  MAUMIVU YA TUMBO MARA KWA MARA


Maumivu haya ya tumbo huweza kumpata mtu wa jinsia yoyote (mwanamke au mwanaume), mtu wa umri wowote(mtoto au mtu mzima), au mtu wa jamii yoyote, na pia maumivu haya huweza kuhusisha, maumivu ya tumbo chini ya kitovu, maumivu ya tumbo upande wa kushoto,maumivu ya tumbo upande wa kulia,maumivu ya tumbo eneo la nyonga,maumivu ya tumbo juu ya kitovu au maumivu ya tumbo katikati ya kitovu.


CHANZO CHA MAUMIVU YA TUMBO LA MARA KWA MARA


Maumivu ya tumbo katika maeneo yote niliyoyataja hapo juu,huweza kuchangiwa na sababu mbali mbali ikiwemo;


1). Uwepo wa tatizo la Hernia au Ngiri


2). Matatizo ya korodani,ikiwemo korodani kushindwa kushuka hasa kwa mtu ambaye tayari umri ni mkubwa


3). Tatizo la vidonda vya tumbo kwa mhusika na hii hutokea mara kwa mara baada ya kula vyakula vyenye acid kali, kama maharage,pilipili n.k


4). Maaumbikizi katia njia na mfumo mzima wa mkojo,au kwa kitaalam Urinary track infection(UTI), hasa hasa watu wenye UTI hupata maumivu ya tumbo upande wa kushoto


5). Kupatwa na tatizo la Kidole tumbo au kwa kitaalam tunaita APPENDIX


6). Kupata matatizo kwenye utumbo mkubwa


7). Kupatwa na shida ya kukosa choo au kupata choo kigumu sana


8). Tumbo kujaa gesi


9). Kupatwa na tatizo la mawe ya Figo kwa kitaalam hujulikana kama Kidney stones


10). Kifuko cha nyongo kupasukia tumboni


11). Kupata matatizo ya Ini


12). Kupatwa na mchafuko wa tumbo ambao huchangiwa na sababu mbali mbali kama vyakula,Vinywaji, Maji, au kula kitu chenye Sumu


13). Kuziba kwa mirija ya Uzazi( blocked Fallopian tubes)


14). Kupatwa na shida ya uvimbe kwenye kizazi au kwenye vifuko vya mayai.


15). Maumivu ya tumbo chini ya kitovu kwa sababu ya HEDHI


16). Kupatwa na shida ya Mimba kutunga Nje ya Kizazi( Ectopic pregnancy)


17). Kupatwa na shida ya Mimba kuharibika


Ni matumaini yangu kwamba angalau umepata picha juu ya vyanzo mbali mbali vya maumivu ya tumbo, japo kwa ushauri zaidi,elimu au tiba tunaweza kuwasiliana kupitia namba +255758286584.

Karibu sana..!!!




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!