DALILI HATARISHI KWA MTOTO MCHANGA AMBAZO UZIONAPO HARAKA FIKA KITUO CHA AFYA


• • • • • •

DALILI HATARISHI KWA MTOTO MCHANGA AMBAZO UZIONAPO HARAKA FIKA KITUO CHA AFYA


Ziko dalili hatarishi nyingi sana ambazo mtoto mchanga anaweza kuwa nazo, na dalili hizi zinaweza kuwa ni moja ya dalili zinazoonyesha tatizo kubwa ambalo yuko nalo mtoto, hivyo basi uzionapo dalili hizi tafadhari usipuuze bali fika haraka katika kituo cha afya ili kupata ufumbuzi wa tatizo hilo. Miongoni mwa dalili ni


1. Kushindwa kunyonya au kukataa kunyonya

2. Kuwa na ngozi ya baridi

3. Kuwa na joto kali/homa

4. Kushindwa kuongezeka uzito au kupungua uzito kulikopitiliza ndani ya wiki moja baada ya kuzaliwa

5. Kutokwa na damu katika sehemu yoyote ya mwili

6. Kupumua haraka haraka

7. Kifua kuzama/kuingia ndani wakati mtoto akipumua

8. Kupumua kwa shida au kutokupumua kabisa 

9. Kuharisha

10. Kutapika kusiko koma

11. Tumbo kujaa/ kuvimba au kuongezeka

12. Kushindwa kutoa haja kubwa (kinyesi)  ndani ya masaa 24 baada ya kuzaliwa

13. Dege dege

14. Kushindwa kutoa haja ndogo (mkojo) ndani ya masaa 48 baada ya kuzaliwa

15. Kitovu kutoa harufu mbaya


Hizi ni miongoni mwa dalili hatarishi, zipo nyingi na ni jukumu la mama, mlezi au muangalizi kumkagha mtoto mara kwa mara ili iwapo atapata dalili hizi aweze kufanyiwa vipimo na kupatiwa matibabu mapema iwezekanavyo.


By Emmanuel Lwamayanga




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!