Ticker

6/recent/ticker-posts

DALILI ZA HATARI AMBAZO HUWEZA KUMPATA MAMA MJAMZITO



MJAMZITO

• • • • • •

Kipindi Cha UJAUZITO  kuna MAMBO ambayo kila MJAMZITO anapaswa KUJUA ili Ikimtokea AJUE hatua ya kuchukua.(mimi nikiwa Kazin huwa nikikutana na Mama k,wengi nawauliza Nione Kama wana hii ELIMU,na kama Hajui Namwelewesha.


Hii itasaidia Sana sanaaa Kupunguza  vifo vya Kina mama vinavyotokana na UZAZI na kupunguza vifo vya watoto  wachanga au watoto wanaozaliwa wamekufa.


Haya mama wajawazito wote,unapokuwa na MIMBA lazima ujue KUTOFAUTISHA dalili,

Kuna dalili za Kulala na kusema nitampigia simu Doctor😀 anishauri na kuna Dalili za Kuita Usafiri na KUWAHI HOSPITALIN📌.


Mfano ukiwa na Kiungulia,utapambana hivo hivo siku itaisha,mafua,kikohozi etc ni vitu vidogo sio vya kukimbizana kwenda Hospitalini.


Dalili Zifuatazo,tena nazipanga KIUZITO,Ukiipata NENDA HOSPITALINI  HARAKA SANA👌📌.


1.Damu Kutoka UKEN,hii ni emergency,alarm nyekundu,Haijalishi ukubwa wa MIMBA kama ni mimba changa au kubwa nenda hospitalini ndugu yangu.

Vifo vya uzazi  vingi chanzo kikubwa ni Wanawake  kupoteza sana Damu.


2.kupata Degedege Ni dalili HATARI pia,inaweza kuwa mama ana kifafa cha mimba ambacho ni hatari sana,unapowahi hospitalin unapata Tiba haraka na kuepukana na madhara makubwa ya Kifafa cha Mimba


3.mtoto asipocheza,tunashauri mama apate mapumziko ajilaze ubavu ubavu asikilizie,ukikuta masaa yanaenda Haujamsikia,Nenda hospitali haraka.


4.KUVIMBA MWILI.

Mimba Ikiwa Kubwa wamama wengi hujaa sana na miguu kuvimba inakuwa Inabonyea ivi na kuacha shimo,ili hali ya kuvimba Ikizidi sana,nenda hospitalin ukachunguzwe haraka sana,presha ikiwa Juu husababisha miguu kuvimba,lakin pia magonjwa ya moyo,figo etc.

Dr wako ndio Akuambie kusema kuvimba kwako ni kwa kawaida baada ya kukuchunguza.


5.Maumivu makali sana ya Tumbo.

Huwa kuna maumivu mama k anaweza pata ya hapa na pale,ila maumivu makali sana sio dalili nzuri, unatakiwa uonwe na mtaalamu wako


6.kichwa KUUMA sana,Kuona giza giza zaweza kuwa dalili za presha iliyopanda,au kifafa cha mimba Kabisa,Unapopata haya embu muone Mtaalamu Uchunguzwe.


Mungu awalinde Mama K wote,safari zenu zikawe zenye baraka,mimba zikafikishe Miez 9 na mkajifungue Salama,watoto wenye afya.


📌Mwanamke ASIPOTEZE UHAI WAKE kwa ajili ya uzazi 📌.


SHARE

Dr.Latifa






Post a Comment

0 Comments