DALILI ZA HOMA YA CHIKUNGUNYA
Dalili za ugonjwa huu huanza kuonekana kati ya siku 3 hadi 7 toka pale mgonjwa ang’atwe na mbu mwenye huyo kirusi
1. Homa(fever): hii ni mojawapo dalili kuu na ya kwanza kutokea,mgonjwa anaweza kua na joto kali la kuanzia 38-39 kwa muda wa siku 3 hadi 5
2. Maumivu ya viungo(anthralgia):
3. Kuvimba viungo(anthritis)
4. Kutokewa na vipele na harara pamoja na malengelenge
5. Mwili kuchoka choka
6. Maumivu ya misuli
7. Maumivu ya kichwa
8. Kichefuchefu na kutapika
NAMNA UGONJWA HUU HUGUNDULIKA
Mgonjwa atahisiwa anaweza kua na ugonjwa wa chikungunya kama anahistoria ya kutoka ama kuishi maeneo yenye mbu wenye mabakamabaka(aedes) na ana dalili tajwa hapo juu. Kama mgonjwa atakuja na mambo hayo basi atafanyiwa vipimo ili kuthibitisha
MATIBABU YA UGONJWA HUU
Ugonjwa wa chikungunya kwa bahati nzuri sio ugonjwa unaoua watu bali utakuletea maumivu makali na hata ulemavu wa kudumu. Mgonjwa atatibiwa kulingana na namna atakavyokuja na mfumo uliathirika. Mgonjwa atapewa dawa za maumivu,atafanyiwa mazoezi ya viungo,atafanyiwa massage,atapewa msaada wa maji ya dawa kulingana na hali ya mgonjwa(supportive treatment), mgonjwa anaweza kuhitaji matibabu makubwa ya mifupa kutokana na uharibifu wa viungo ambavyo anaweza kuupata kama matokeo ya ugonjwa huu.
Kwa bahati nzuri sana wagonjwa wote wa chikungunya hupona na kwenda nyumbani .
.
Itaendelea..
.
.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!