DALILI ZA KUOTA MENO KWA MTOTO
MENO
• • • • • •
Watoto wengi huanza kuota meno kati ya umri wa miezi 4-7. Lakini baadhi huanza mapema zaidi .
.
DALILI ZA KUOTA MENO KWA WATOTO
Dalili huweza kutofautiana baina ya watoto mbalimbali, dalili ni kama;
1. Fizi kuvimba na kuuma
2. Mtoto kulia na kutokutulia
3. Homa kiasi
4. Mtoto kung'atang'ata vidole ama kujaribu kutafuna vitu
5. Mtoto kutokwa mate kwa wingi
6. Mabadiliko katika ulaji na ulalaji .
.
Kuota meno huweza kuleta maumivu kwa watoto lakini hiyo haiwafanyi wao KUWA WAGONJWA. Ila kama mwanao anaharisha, kutapika, kutokwa upele, homa kali, au kikohozi MUONE DAKTARI kwani hizi si dalili za kawaida za kuota meno .
.
NINI CHA KUFANYA?
Sio kila anachofanyiwa mtoto fulani basi kwa mtoto mwingine kitaleta ahueni
1. Mfanyie masaji ya fizi mtoto kabla meno hayajatokeza kwa kuzungushia gauze/kitambaa safi na laini kidoleni na kusugua taratibu fizi zake
2. Mara kadhaa, vitu vyenye ubaridi kiasi husaidia pia kama kijiko cha plastiki kilichowekwa katika friji kwa muda mfupi na chenye ubaridi wa wastani(usioweza kumuathiri mtoto) ama toy zake za kuchezea. Hakikisha ni visafi na salama kabla ya kumpa ang'ate
3. Watoto wanaoota meno hupendelea kung'ata vitu mbalimbali hivyo muache atafune kadri awezavyo ILA tu hakikisha ni safi na salama
4. Kama mwanao ana zaidi ya miezi 6 unaweza kumpa maji yenye baridi la wastani(yaliyo safi na salama) katika kijiko safi, hii pia husaidia
5. Pia, unaweza mpa kidole chako kisafi ajaribu kung'atang'ata kwani huwa inasaidia pia
VIPI KUHUSU KUMPA MTOTO DAWA?
Dawa nyingi utakazo msugua mwanao maeneo ya fizi ili kupunguza maumivu mara nyingi hazisaidii, kwa sababu husombwa na mate na kuisha. Lakini unaweza kumuwekea karafuu iliyosiginwa Kwani ni ya asili na husaidia
Kaa mbali na dawa za jelly au za maji zenye kemikali ya BENZOCAINE. Kitaalamu kemikali hii haifai kwa matumizi ya watoto wenye chini ya umri wa miaka 2 Kwani huweza kuleta madhara makubwa
Unaweza kumpa dozi ya Paracetamol ili kupunguza maumivu. Lakini hakikisha ameandikiwa na Daktari .
MUHIMU: Mtoto kuota meno huweza kuwanyima raha familia nzima lakini taratibutaratibu unavyotambua njia ipi inamfaa mtoto kupunguza maumivu basi mambo huwa SHWARI!!! #afyabongo #drtareeq
.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!