UTI
• • • • • •
Dalili za maambukizi ya mfumo wa mkojo ni zipi?
Dalili hutofautiana kulingana na ukali wa maambukizi,umri na sehemu iliyoathiri..
Dalili zinazojitokeza mara nyingi pakiwa na maambukizi (UTI):
📍Uchungu au kuwashwa unapokojoa.
📍Kuhisi kukojoa mara nyingi.
📍Homa na uchovu .
📍Mkojo wenye harufu mbaya na si safi (cloudy).
Dalili zinazotokana na maambukizi ya kibofu
📍Maumivu katika upande wa chini wa tumbo.
📍Kukojoa mkojo kidogo , wenye maumivu na mara nyingi.
📍Dalili za homa kidogo. Bila maumivu ya mbavu.
📍Damu kwenye mkojo.
Dalili zinazotokana na maambukizi ya upande wa juu wa njia ya mkojo
📍Maumivu ya upande wa juu wa mgongo na mbavu.
📍Kuwa na homa na kuhisi kibaridi. Kichefuchefu, kutapika, uchovu na kujihisi mgonjwa kwa ujumla.
📍Kuchanganyikiwa kwa wazee.
Maambukizi haya ni hatari sana yasipotibiwa vyema na haraka. Aidha yanaweza hata kuhatarisha maisha.
0 Comments