DALILI ZA MTU MWENYE SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI


DALILI ZA MTU MWENYE SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

Wanawake wengi hawana dalili,kwa hiyo ni muhimu kucheki shingo yako ili ujue ikoje

Kutokwa na maji maji mepesi yenye au yasiyo na damu yenye harufu ya kipekee.

Kutokwa na damu wakati na baada ya kufanya tendo la ndoa

Kukojoa damu(imeshasambaa hadi kenye kibofu cha mkojo)

Shida ya kupumua(imeshasabaa hadi kenye mapafu)

Upungufu wa damu(imeshasabaa hadi kenye mifupa)

Kuchanganyikiwa na degedege(imeshasabaa hadi kenye ubongo)

Mkojo kutokea njia ya haja kubwa  au choo kutokea njia ya mkojo


MOTOKEO YA KANSA HII INATEGEMEA NA USAMBAAJI WAKE/HATUA ILIYOPO(STAGE)

Kama ilivyo kwa saratani zingine,matokeo ya saratani hii hutegemea a hatua ya uugonjwa kwa wakati ule.kama ugonjwa upo hatua za mwanzoni hatua ya I na II matokeo yake sio mabaya kama ikiwa hatua ya III na IV ambayo matokeo yake n mabaya.kwa walio stage I nafasi ya kuishi miaka mitano ni Zaidi ya asilimia 90,walio stage II nafasi ya kuishi miaka mitano ni kati ya asilimia 60-80,walio stage III nafasi yao ya kuishi miaka  ni asilimia 50 na walio stage IV nafasi ya kuishi miaka mitano ni chini ya asilimia 30 kwa maana nyingine hufa mwaka huo huo alogundulika.


NAMNA YA KUJIKNGA NA HUU UGONJWA

Kupima shingo yako na kajua hali yako

Punguza wapenzi ulio nao au achana nao kabisa

Matumizi ya kondomu kila tendo na kwa usahihi

Kujishughulisha na kazi mbalimbali za kujipatia kipato

Acha kuvuta sigara

Watoto wa kike wasianze mapenzi wakiwa na miaka chini ya 20

Pata chanjo ya HPV ili kujilinda na saratani hii(utapata chanjo hii kama hujawahi kukutana na mwanaume pekee)

Kupima VVU na kutumia dawa kama umeambukizwa HIV.

.

Itaendelea.

Follow @neema_b_mrosso 

@cdeglory 

@cdeglory @cdeglory.

.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!