DALILI ZA UGONJWA WA KISUKARI

 DALILI ZA KISUKARI


Kabla ya kujua dalili za ugonjwa huu wa kisukari, hebu tuangalia kidogo kuhusu vihatarishi vya kupata tatizo hili.

Vihatarishi hivo ni pamoja na;


- Kupendelea kula vyakula vya sukari nyingi


- Unywaji wa Pombe sana


-  Utumiaji wa baadhi ya mafuta ya kula


- Kwa ujumla wake mtindo mzima wa maisha au Lifestyle huweza kuchangia pia mtu kupatwa na ugonjwa kisukari


- Kongosho lenyewe kufeli au kushindwa kufanya kazi


- Unene au kuwa na uzito mkubwa sana


- Ulaji wa vyakula vya mafuta sana


- Kutokuushuhulisha mwili wako


- Kuna swala pia la umri


- Tatizo la presha pia huweza kusababisha mtu kupata ugonjwa wa kisukari


DALILI ZA UGONJWA WA KISUKARI

Dalili za kisukari ni pamoja na;


  • Uzito kupungua sana
  • Kupatwa na shida ya kukojoa kojoa mara kwa mara
  • Kuwa na njaa sana mara kwa mara
  • Kupatwa na shida ya kutokuona vizuri
  • Kupata kiu sana
  • Kupata uchovu sana wa mwili
  • Kupatwa na Ganzi miguuni pamoja na kwenye Mikono
  • Kushindwa kuhimili tendo la Ndoa vizuri

Kama una Dalili hizi, kutana na wataalam wa afya kwa ajili ya Vipimo na Msaada wa kimatibabu



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!