🔻DALILI ZA UVIMBE KWENYE KIZAZI
Kama nilivokwisha kusema hapo juu ni kwamba wanawawake wengi wana uvimbe kwenye kizazi na jambo zuri ni kwamba hawaonyeshi dalili kwa asilimia kubwa. Wanawake walio wengi hugundulika na uvimbe kwenye kizazi pale wanapokwenda kufanya check up ya vitu vingine na ndipo hugundulika na myoma(found incidentally on pelvic imaging). Kama mwanamke mwenye uvimbe kwenye kizazi atapata dalili basi anaweza kupata mambo yafuatayao:-
1) kutokwa na damu nyingi ya hedhi au isiyokata mapema(Heavy or prolonged menstrual bleeding). Hi ni mojawapo ya dalili kuu ambayo mwanamke huipata,mwanamke anaweza kutokwa na damu nyingi sana mpaka ikapelekea kupata upungufu wa damu unaohitaji kuongezewa damu,wakati mwingine hedhi inaweza ikachukua muda mrefu kukata mfano hedhi inaweza kuchukua mpaka siku 15 bila kukata.
2) Maumivu wakati wa hedhi(Dysmenorrhea)
3) Maumivu ya nyonga na kiuno pamoja na kua na uzito kwenye nyonga(Pelvic pressure or pain )
4) Maumivu wakati wa kufanya mapenzi(dyspareunia)
5) Matatizo ya kubeba ujauzito/ugumba(difficulty conceiving a pregnancy)
6) Mimba kuharibika mara kwa mara(miscarriage
7) Mtoto kudumaa akiwa tumboni(fetal growth restriction)
8) Matatizo ya kukojoa(Urinary symptoms);wakati mwingine mwanamke mwenye uvimbe kwenye kizazi hasa uvimbe mkubwa anaweza akawa anakojoa mara kwa mara mchana au kushindwa kukojoa au kutoa mkojo wote;hii inatokana na kama uvimbe ni mkubwa na unakandamiza kwenye kibofu cha mkojo
9) Matatizo ya kupata choo(Bowel symptoms);wakati mwingine mwanamke mwenye uvimbe kwenye kizazi hasa uvimbe mkubwa anaweza akawa na matatizo ya kushindwa kupata choo mara kwa mara au kupata choo kigumu au kuharisha;hii inatokana na kama uvimbe ni mkubwa na unakandamiza kwenye mkundu(pressure on the rectum)
10) Kupata uchungu kabla ya siku na kujifungua kabla ya wakati(preterm labor and birth)
11) Kondo la nyuma kuachia(placental abruption)
12) Mtoto kukaa vibaya tumboni(malpresentation)
.
.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!