DONDOO ZA UJAUZITO NA DALILI ZA HATARI UKIWA MJAMZITO

DALILI HIZI ZINATAKA UCHUKUE HATUA MAPEMA


1. Kuchoka, kukosa pumzi pamoja na kizunguzungu.

2. Kutokwa damu ukeni.

3. Kupasuka chupa kabla ya uchungu.

4. Maumivu makali ya kichwa na kuona giza machoni.

5. Kutokwa na majimaji yenye harufu ukeni.

6. Mlalo mbaya wa mtoto tumboni baada ya wiki ya 36 ya ujauzito. 

7. Kupungua au kutocheza kabisa kwa mtoto tumboni. 

8. Maumivu makali sehemu ya chini ya tumbo.


KUMBUKA

•Kila ujauzito ni hatari kwa maisha ya mama na mtoto.

•Ukiona ishara moja tu ya hatari wakati wa ujauzito nenda haraka kituo cha huduma ya afya.

•Kama ifikapo wiki ya 41 hujajifungua, nenda mara moja kituo cha Huduma ya Afya. 

.Drtareeq

.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!





0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!