UNYONYESHAJI
• • • • • •
Kunyonyesha kuna faida nyingi sana kwa mtoto mchanga pia na kwa mama. Tuanze na faida kwa mtoto:
1. Virutubisho vilivyomo kwenye maziwa ya mama ni muhimu kwa mtoto mchanga , maana maziwa ya mama huwa na uwiano mzuri wa vitamin, protini, na mafuta mazuri na kumuwezesha mtoto kukuwa vizuri
Vilevile maziwa ya mama huwa na virutubisho vyenye uwezo wa kumkinga mtoto kupata magonjwa, kitaalamu 'antibodies', ambavyo humkinga mtoto mchanga dhidi ya vimelea (bakteria na virusi)
• • • • • •
Maziwa ya mama hupunguza uwezekano wa mtoto mchanga kupata pumu au aleji
Na vilevile watoto wakinyonyeshwa kwa miezi sita mfululizo bila kuchanganyiwa na vyakula vingine hupunguza hatari ya kupata maambukizi ya masikio, mfumo wa hewa na magonjwa ya kuharisha
• • • • • •
Faida za kunyonyesha kwa mama ni kama zifuatazo:
-Husaidia kupunguza uzito kwa mama hasa baada ya kujifungua
-Husaidia kutolewa kwa kichochezi Oxytocin ambacho husaidia kurudisha mfuko wa kizazi katika size yake ya zamani kabla ya ujauzito
-Husaidia kupunguza hatari ya saratani za matiti na ovary, pia hupunguza hatari za matatizo ya mifupa
-Husaidia kuwa karibu na mtoto (bonding)
Inashauriwa Mama kumnyonyesha mtoto pale anapohisi kuwa ana njaa. Wengi wamekuwa wakitegemea kumsikia mtoto analia kama ishara ya njaa, lakini kulia ni ishara ya mwiho ya njaa, ina maana mpaka analia itakuwa ameshasikia njaa na ameshindwa kuvumilia. Zifuatazo ni baadhi ya ishara kuwa mtoto ana njaa (anahitaji kunyonyeshwa)
-Anazungusha kichwa huku na huku
-Anaachama mdomo
-Anang'atang'ata ulimi kama anamung'unya kitu
-Anakula vidole
-Analamba midomo
-Anajaribu kushikashika vitu
-Ishara nyingine hutegemeana na mtoto, hivyo kama mama, unatakiwa uhakikishe umezizoea na kujua ishara kuu za mtoto wako.
• • • • • •
Ninajuaje kama mtoto hapati maziwa ya kutosha? Swali hili ni moja ya maswali ambayo wamama wengi wamekuwa wakijiliza, je nitajuaje kama mtoto anapata maziwa ya kutosha. Zifuatazo ni baadhi ya ishara kuonesha kuwa mtoto hapati mawiwa ya kutosha
-Unamuona anakuwa hajatosheka hata baada ya kunyonya
-Anakuwa na njaa kwa vipindi vifupivifupi sana
-Anapata choo au mkojo mara chache saaana
-Ana hasira na ana lialia sana
-Haongezeki uzito
Endapo utaona dalili hizi, zingatia kwenda hospitali au wasiliana na daktari wako kwa ushauri zaidi ili kuweza kupata suluhisho.
• • • • • •
Ni muhimu kufahamu, Unyonyeshaji hauchangii maziwa kulala wala kuharibu umbo la maziwa
Sababu kuu za maziwa kulala ni
1️⃣Umri
2️⃣Vinasaba vya urithi
3️⃣Unene wako wa mwili
4️⃣Utapiamlo hasa upungufu wa vitamin C
5️⃣Kuvuta sigara
6️⃣Kujifungua mara nyingi
Kuhusu kubeba ujauzito mara nyingi, Mama anapokuwa mjamzito maziwa hupitia mabadiliko kama kuongezeka ukubwa na umbo,
Baada ya kujifungua umbo hurudi lilivyokuwa kabla lakini huwa tofauti kidogo. Mabadiliko haya hutokea kila ujauzito, mwisho maziwa hulala na sio sababu ya kunyonyesha
Vitamin C hutengeneza Collagen malighafi muhimu kwenye ngozi na kiwambo kinachoshika maziwa.
Iwapo mwanamke hapati Vitamin C ya kutosha ngozi na kiwambo cha maziwa huwa dhaifu na maziwa hulala.
Vitamin C hupatikana Kwa wingi kwenye machugwa, chenza, viazi lishe nk
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!