FAHAMU ATHARI ZA BAADHI YA MAKUNDI YA DAMU KWA MTOTO ANAYEZALIWA
NAMNA MAKUNDI HAYA HUATHIRI UZAZI NA AFYA YA MTOTO
Wanawake wanaopata matatizo haya ya uzazi na adhari kwa mtoto ni wale ambao makundi yao ya damu hayana rhesus factor au tunasema Rhesus Factor Negative(rh-ve), mfano; ukisema una Group la Damu A-ve, B-ve, n.k.na waume zao wana hizo rhesus factor au tunasema Rhesus Factor Postive(rh+ve) mfano; ukisema una group la Damu A+ve, B+ve n.k.
KWA MFANO; Baba ana group la Damu A+ve na Mama B-ve
Matatizo mara nyingi hayaanzii katika ujauzito wa kwanza bali huanza ujauzito wa pili na kuendelea kwa sababu katika ujauzito wa kwanza mwili wa mama ulikua bado unajiandaa kutengeneza kingamwili(antibodies) kwa ajili ya kupambana na hiyo rhesus factor ambayo ulinzi wa mwili umeitafsiri kama mvamizi ama mgeni.
Wanawake wengi kwa namna moja ama nyingine hawalijui hili na huanza kupata mshangao na hata kuanza kua na mawazo potofu juu ya hali yake kwa sababu mimba ya kwanza imeenda vizuri lakini kuanzia ya pili nay a kuendelea ni aidha mimba zinaharibika,mtoto kufia tumboni au kufariki saa au siku chache baada ya kuzaliwa.
Ikumbukwe kwamba mchanganyikano wa damu ya mama na mtoto hutokea aidha akiwa bado yuko tumboni au wakati mtoto anazaliwa,kuchanganyika kwa damu hupelekea rhesus factor kuingia kwa mama na ndipo kingamwili hutengenezwa kwa ajili ya mapambano na hivo basi endapo mimba nyingine ikiingia ya baba Yule Yule basi zile kinga mwili zitaingia kwa mtoto na kuanza kushambulia chembechembe zake za damu na kumpelekea mtoto kupata upungufu mkubwa wa damu na magonjwa ya moyo akiwa tumboni. Kama nilivosema hapo awali hii hutokea kuanzia ujauzito wa pili iwe umejifungua kawaida,kwa operesheni,mtoto amefia tumboni au mimba imetoka au umetoa mimba na ili hali damu yako haina rhesus factor basi jua ni lazima uchukue tahadhari kama unataka kupata uzazi usio na matatizo huko mbeleni.
@ Kama Hujaelewa Maelezo haya tuwasiliane inbox ili nikueleweshe vizuri.
.
.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!