MAZIWA
• • • • • •
FAHAMU FAIDA ZA MAZIWA NA VYAKULA VIONGEZAVYO UTENGENEZAJI WA MAZIWA.
Maziwa ya mama kwa mtoto yanafaida nyingi sana ikiwemo kinga na virutubisho vinavyomsaidia mtoto kukua. Kitaalamu inashauriwa mtoto anyonye pasipo kuchanganyiwa kitu kingine kwa muda usiopungua miezi sita na baada ya miezi sita mama anaruhusiwa kuongeza vyakula laini na huku akiendelea kumnyonyesha. Maziwa ya mama yanakila kitu ambacho mtoto anatakiwa kupata ndani ya miezi sita ya mwanzo ikiwemo maji, protini, vitamin, madini mafuta na kinga za mwili. Hivi vyote uchangia katika ukuaji wa mtoto.
FAIDA ZA MAZIWA YA MAMA KWA MTOTO.
1. Zinachangia ukuaji na kumkinga mtoto na magonjwa
2. Yanasaidia mahusiano mazuri ya mama na mtoto pamoja na kumkinga na baadhi ya allergy.
3. Maziwa ya mama yanameng’enywa kwa urahisi ukilinganisha na maziwa au vyanzo vingine vya chakula.
FAIDA ZA KUNYONYESHA KWA MAMA
1. Inapunguza hatari ya kupata saratani ya ovari na matiti.
2. Inasaidia nyumba ya uzazi kurudi haraka katika hali yake ya kawaida
3. Inapunguza hatari ya kupoteza damu nyingi baada ya kujifungua lakini pia inamsaidia mama kupunguza uzito ambao huongezeka wakati wa mimba
3. Hayana gharama ukilinganisha na vyanzo vingine vya maziwa au chakula.
VYAKULA VINAVYOONGEZA UTENGENEZWAJI WA MAZIWA.
Wanawake wengi wanekuwa wakulalamika au kukubwa na tatizo la kutokutengeneza maziwa ya kutosha na hivyo kupelekea ukuaji hafifu wa watoto wao. Vifuatavyo ni vyakula na matunda yaongezayo utengenezaji wa maziwa.
1. Mboga za majani kama spinachi na matembele
2. Vitunguu swaumu na tangawizi. Mbali na kuongeza radha ya chakula viungo hivi vinaaminika kwa kuongeza utengenezaji wa mazima.
3. Siagi ya karanga
4. Viazi vikuu, viazi vitamu, karoti na mapapai
5. Maziwa ya ng’ombe, maji mengi na juisi ya kutengeneza
6. Mbegu za mikunde kunde (zina protini nyingi)
7. Mayai na nyama( kama supu ya kuku)
8. Parachichi (avocado)
9. Mafuta ya samaki
10. Nafaka na vyakula vya wanga kama mkate, mtama, mahindi na vyakula vya ngano.
SABABU ZINAZOPELEKEA UPUNGUFU WA MAZIWA.
1. Kutokunyonyesha mara kwa mara hasa hasa wakati wa usiku.
2. Kuchelewa kuanzisha unyonyeshaji wa mtoto.
3. Uwekaji mbaya wa mtoto katika ziwa
4. Matumizi ya chupa
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!