POMBE
• • • • • •
FAHAMU KUHUSIANA NA ATHARI ZA POMBE NA ULEVI ULIOPINDUKIA.
pombe iingiapo mwilini husambaa ktk mwili mzima na huathiri kila mfumo mwilini, huzidisha makali ya magonjwa na huathiri utendaji kazi wa dawa mbalimbali.
Uwezekano wa kupata madhara yatokanayo na pombe ni 20% kwa mwanaume na 10% kwa mwanamke ktk maisha yake yote. Madhara haya upunguza mpaka miaka 10 ya kuishi kwake duniani.
Pombe hufyonzwa/hunyonywa ktk kiwango kidogo mdomoni na koo la chakula, kiwango cha kati katika tumbo na utumbo mpana na kwa kiwango kikubwa katika sehemu ya juu ya utumbo mwembamba. Asilimia kadhaa hutolewa kwa njia ya mapafu, mkojo na jasho na inayobaki hubadilishwa kuwa acetyladehyde ambayo huaribiwa haraka na kemikali za mwili.
Pombe huathiri visafirishi (neurotransmitters) kama GABA, NMDA, dopamine na serotonin na hivyo kupelekea athari kisaikolojia, kifisiolojia na kitabia.
Mabadiliko ktk utambuzi na tabia hutokea ikiwa kiwango cha pombe ktk damu ni kati ya 0.02-0.04g/dl na kifo hutokea iwapo imefikia 0.30-0.40g/dl
FAIDA ZA POMBE
Pombe ktk kiwango kidogo,
1. kinaongeza kiwango cha cholesterol nzuri mwilini
2. Kupunguza mkusanyiko wa visahani vya damu na hivyo kupunguza uwezekano wa matatizo ya moyo
ATHARI ZA POMBE
a) mfumo wa fahamu
1. Kupoteza kumbukumbu za kile kilichotokea baada ya kunywa
2. Kukosa usingizi
3. Kukoroma
4. Ndoto mbaya usingizini
5. Kutokuwa na maamuzi sahihi na kukosa ushirikiano ktk sehemu za mwili
6. Miguu kufa ganzi
7. Matatizo ktk mfumo tambuzi
8. Maumivu ya kichwa, kiu, kichefuchefu, na kuchoka siku inayofuata baada ya kunywa (hangover)
B) matatizo ya akili
Pombe huweza kuchochea au kuhamsha magonjwa ya akili
C) mfumo wa mmeng'enyo wa chakula
1. Kutokwa na damu
2. Kushuka kwa kiwango cha sukari mwilini
3. Matatizo ktk ini
D) saratani
E) mfumo wa mzunguko wa damu
1. Matatizo ya moyo
2. Shinikizo la damu
3. Kupungua kwa utengenezwaji wa sele nyeupe za damu, inapunguza uwezo wa udundaji wa moyo
F) mfumo wa uzazi
a) mwanaume
1. Kupungua kwa uwezo wa kusimamisha uume
2. Kusinya/kukonda kwa korodani
3. Kupungua kwa mbegu za kiume
b) mwanamke
1. kutokuingia hedhi
2. Kuharibika mimba
3. Ugumba
By Emmanuel Lwamayanga.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!