FAHAMU KUHUSIANA NA FANGASI UKENI

FANGASI

• • • • • •

FAHAMU KUHUSIANA NA FANGASI UKENI. 


fangasi kwa wanawake limekuwa ni tatizo linalowakumba wanawake wengi hasa kati ya miaka 20-40. 20% ya wanawake wana fangasi hawa lakini hawaoneshi dalili yoyote. 


Asimia 90% ya maambukizi ya fangusi katika uke yanasababishwa na fangasi ambae kitaalamu anafahamika kama candida albicans.  Asilimia zilizobaki husababishwa na aina nyingine ya fangusi na fangasi hawa wakawaida ya kusababisha maambukizi ya kujirudia rudia mara baada ya matibabu.  Baadhi ya wanawake wamekuwa na maambukizi zaidi ya mara nne ndani ya mwaka mmoja. 


Fangasi huyu hupatikana katika maeneo ya tofauti ya mwili kama kiumbe rafiki.  Maeneo haya ni kama mdomoni,  maeneo ya utumbo(rectum) pamoja na uke.  Fangasi hawa huweza kusambaza kwa njia ya kujamiiana na ziko tafiti zinazoonesha uhusiano wa ugonjwa huu na ufanyaji wa mapenzi unaohusisha sehemu za siri na mdomo. 


VIHATARISHI

1. kisukari 

2.  Ujauzito/mimba 

3.  Matumizi ya dawa zitumikazo kuuwa vijidudu mwilini 

4. Vidonge vya panga uzazi (japo tafiti bado zinaendelea juu ya hili) 

5. Kushuka kwa kinga ya mwili (UKIMWI,  saratani nk) 

6. Madawa mbalimbali 

7. Magonjwa ya tezi ya thyroidi na parathyroidi 

8.  Uzito uliopitiliza/ kilibatumbo. 


DALILI

1. kuwashwa maeneo mbalimbali ya uke 

2. Kutokwa na uchafu mweupe mzito mithiri ya maziwa mgando ambao wakati mwingine ugandia katika kuta za uke na iwapo utatolewa upelekea kuvuja kwa damu 

3. Maumivu wakati wa tendo la ndoa 

4. Uke kuonekana kuvimba na kuwa na sehemu nyekundu nyekundu 

5.  Kuvimba kwa sehemu ya nje ya uke 

6. Kuchubuka katika maeneo mbalimbali ya uke 


NINI KIFANYIKE

1. mwamamke anashauriwa kutokutumia sabuni,  marashi ktk sehemu za siri au nguo za ndani zilizotengenezwa ka mipira. 

2. Kupunguza matumizi ya dawa yasiyo ya lazima na watumie dawa ikiwa tu wamepewa na kuelekezwa na mtoa huduma. 

3. Hakikisha sukari yako inakaa sawa. 

4. Fanya mazoezi na ule vizuri kuepusha ongezeko la uzito lililopitiliza. 


Afya ni kitu bora zaidi 

By Emmanuel Lwamayanga




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!