FAHAMU KUHUSIANA NA FISTULA

FISTULA

• • • • • •

FAHAMU KUHUSIANA NA FISTULA


FISTULA ni shimo/kitundu au uwazi usiosahihi unaounganisha sehemu mbili katika mwili. Zipo aina nyingi za fistula ila kwa leo nitazungumzia fistula inayotokea kati ya kibofu cha mkojo na sehemu ya siri ya mwanamke(uke) kitaalamu inaitwa (vesicovaginal fistula). Fistula imekuwa ni moja ya matatizo yanayowakumba kina mama na kumekuwa na ongezeko hivi karibuni hii ni kutokana na kuongezeka kwa mimba za utotoni, kuongezeka kwa upasuaji na sababu nyingine nyingi. Fistula husababisha athari nyingi katika jamii ikiwemo za kiuchumi, kijamii na hata kisaikolojia.


NINI HUSABABISHA FISTULA?

1. Uzazi pingamizi

Katika nchi zinazoendelea kama Tanzania, fistula imekuwa ikisababishwa na uZazi pingamizi. Katika uzazi pingamizi mtoto hushindwa kushuka katika nyonga hali hii hupelekea kichwa cha mtoto kukandamiza viungo vilivyo kwenye nyonga ikiwemo kibofu cha mkojo. Mkandamizo huu huzuia damu kufika eneo hili na kupelekea seli kufa. Vijidudu huota pale na hivyo kusababisha kumeguka au kumomonyoka kwa vinyama sehemu ile na hivyo kutengeneza kitundu kinachounganisha sehemu hizo mbili yaani kibofu cha mkojo na uke. Mara nyingi fistula hutokea kati ya siku ya 3-5 baada ya kujifungua.


Sababu nyingine ni

2. Upasuaji wa uzazi au kuzalishwa kwa vifaa

3. Kutibiwa kwa kutumia dozi kubwa ya mionzi

4. Ajari- kuangukia kitu chenye ncha kali ambacho kinaweza toboa kibofu cha mkojo na sehemu mbalimbali za mfumo wa uzazi wa mwanamke

5. Saratani ambayo huweza shambulia sehemu mbalimbali za nyonga na hivyo kupelekea fistula

6. Maambukizi kama TB katika uke, na kichocho.


Mara nyingi fistula huwapata wanawake wanaobeba mimba katika umri mdogo ambao pia wapo kwenye hatari ya kupata uzazi pingamizi.


DALILI ZA FISTULA,

1. Kutokwa na mkojo ukeni pasipo hiari/pasipo kujua

2. Kubabuka/kuungua kwa ngozi inayozunguka sehemu za siri.

3. Kutokuona siku zako za hedhi au hedhi kuvurugika mpangilio.

4. Kuchechemea kutokana na kuharibiwa kwa mishipa ya fahamu(nerves) wakati wa uzazi pingamizi.


MATIBABU YA FISTULA,

-upasuaji


KUJIKINGA,

1. Zuia mimba za utotoni

2. Maudhurio mazuri ya kliniki wakati wa ujauzito

3. Kuwekwa mpira wa mkojo kabla/baada ya kujifungua


By lwamayanga




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!