FAHAMU KUHUSIANA NA ULE UTANDO KAMA MAFUTA AMBAO HUONEKANA KWENYE NGOZI YA MTOTO BAADA YA KUZALIWA.

UTANDO

• • • • • •

FAHAMU KUHUSIANA NA ULE UTANDO KAMA MAFUTA AMBAO HUONEKANA KWENYE NGOZI YA MTOTO BAADA YA KUZALIWA.

(Nimetumia neno utando kwani ndio neno rahisi na linaloeleweka)


Vernix caseosa ni kama utando wenye mafuta mafuta ambao hufunika ngozi ya mtoto katika kipindi cha miezi mitatu ya mwisho ya ujauzito. Tezi ya sebaceous inahusishwa katika utengenezwaji wake.


Utando huu husaidia maboresho ya ngozi ya mtoto awapo tumboni lakini pia husaidia ngozi kuweza kuhimiri mabadiliko ya nje mara mtoto azaliwapo.


Inasadikika kuwa utando huu unapatikana kwa binadamu pekee.


NAMNA AMBAVYO VERNIX CASEOSA UTENGENEZWA.


Katika wiki ya 11 mara baada ya mimba kutungwa, epidermis ambayo ni sehemu ya nje ya ngozi huwa na kuta tatu na kuta ya nje kabisa huitwa periderm. Kutokana na sifa za ukuta huu, periderm husaidia kumlinda mtoto akiwa kwenye yale majimaji ndani ya mji wa mimba lakini pia usaidia katika usafirishaji wa maji na vitu stahiki kati ya mtoto na sehemu ya nje.


Seli zinazojenga ukuta wa periderm huendelea kubadilishwa na mpaka kufikia wiki ya 21 huwa zimekwisha kutolewa na kuota kwa stratum corneum. Zile seli za periderm ambazo zimetolewa kwenye ngozi huungana na mafuta mafuta ambayo hutengenezwa na tezi ya sebaceous na hivyo kutengeneza huu utando unaoitwa vernix caseosa.

Mfumo wa homoni pia unahusishwa katika utengenezwaji wake. 


Vernix caseosa huundwa na 

1. Maji (81%)

2. Mafuta (9%)

3. Protini (10%)


KAZI YA UTANDO HUU (VERNIX CASEOSA)

1. Kusaidia kuboreka kwa mfumo wa chakula. 

2. Hulinda ngozi ya mtoto awapo tumboni na hivyo kuzuia mtoto asichubuke au kubabuliwa na maji yanayomzunguka

3. Wakati wa kuzaliwa utando huu hupunguza msuguano na hivyo hupunguza uwezekano wa mtoto kuumia.

4. Kutunza joto la mwili hasa kwa watoto njiti (tafiti bado zinaendelea juu ya hili)

5. Kulinda mtoto zidi ya maambukizi

6. Kulainisha ngozi (kuipa unyevunyevu)

7. Husaidia ngozi kujisafisha

8. Kutokana na sifa zake inaweza tumiwa kutibu vidonda na kutibu watu walioungua


Shirika la afya dunia (WHO) linashauri kuwa utando huu usifutwe kwenye ngozi ya mtoto mara baada ya kuzaliwa. Kwa kawaida utando huu utoka wenyewe mpaka siku ya mpaka siku ya 5 mara baada ya kuzaliwa.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!