FAHAMU KUHUSIANA NA KUFA KWA UBONGO (BRAIN DEATH)
UBONGO KUFA
• • •
FAHAMU KUHUSIANA NA KUFA KWA UBONGO (BRAIN DEATH)
Kitaalamu kifo kimegawanyika katika aina mbili. Kuna somatic death na cellular death. Kifo cha kisomatic ni hali isiyorudishika/isiyobadilika ambapo mtu hupoteza utu, fahamu au ufahamu wa mazingira, kupoteza uwezo wa kuhisi vichocheo mbalimbali kama maumivu nk, au kupoteza uwezo wa kufanya matendo ya hiari.
Kifo cha seli (cellular death) hii ni hali ambayo tishu na seli zake zinakufa na hivyo kupoteza uwezo wake wa kufanya kazi.
Kifo cha kisomatic kinalinganishwa na kufa kwa ubongo (brain death). Ziko sababu nyingi zinazoweza pelekea ubongo kushindwa kufanya kazi ikiwemo ukosefu wa oksijeni, ajari, au sumu. Iwapo sehemu ya ubongo inayohusika na upumuaji (brainstem) haitokuwa imedhurika basi mtu huyu ataendelea kupumua na hivyo mapigo ya moyo kuzunguka kwa damu mwilini kutaendelea kama kawaida. Lakini mtu huyu atakuwa amepoteza fahamu kabisa. Na anaweza kuwa katika hali hiyo hata kwa miaka japokuwa maambukizi au kukakamaa kwa misuli au kuoza kwa ngozi kunaweza fupisha maisha yake.
Iwapo kuharibika kwa ubongo kutatapakaa na kuhusisha sehemu ya ubongo inayohusika na upumuaji mtu huyu anaweza pata kifo cha seli hivyo watu hawa huwekwa kwenye mashine za kuwasaidia kupumua.
Mijadala bado inaendelea kuhusiana na uamuzi je mtu akiwa na kifo cha ubongo basi ahesabike kuwa amekufa kabisa au aendelee kupewa huduma nyingine kama vyakula nk.
Wako watu ambao wamekuwa katika hali hiyo na wamekuwa wakipumua wakitumia mipira na familia zao ndizo uhusika kutoa uamuzi iwapo watu hawa watolewe kwenye mashine za kusaidia kupumua au lah.
By Emmanuel Lwamayanga
.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!