KUWASHWA SEHEMU ZA SIRI
• • • • • •
FAHAMU KUHUSIANA NA KUWASHWA KWA SEHEMU ZA SIRI ZA MWANAMKE
Takriban asilimia 10 ya wagonjwa ambao huudhuria kliniki ya kina mama huwa na tatizo hili.
Kuwashwa huku huwa zaidi wakati wa usiku kutokana na kutulia kwa akili, kuchoka kwa mfumo wa fahamu joto na kukosekana kwa hewa maeneo hayo.
SABABU
1. Majimaji au uchafu kutoka ukeni usababishwao na trichomonas vaginalis au fangasi
2. Michubuko sehemu za siri
3. Maambukizi
-virusi kama herpes genitalis na vinyama sehemu za siri
-minyoo
-kisonono
4. Allergy- kuvaa nguo za ndani zenye nylon au kufua nguo hizo kwa sabuni yenye kemikali, condom na madawa
5. Kisukari- hupelekea mabadiliko ktk ngozi inayopelekea muwasho lakin pia mabadiliko hayo huchochea fangasi kuota
6. Upungufu wa madini chuma, folic acid, na vitamini A na B 12
7. Matatizo ya kisaikolojia
8. Magonjwa ya tezi ya thyroid
9. Saratani
UTAFITI/UCHUNGUZI
Damu, uchafu kutoka sehemu za siri, mkojo na choo hupimwa ili kutafuta chanzo cha tatizo na kwa baadhi kinyama hutolewa ili kupimwa.
MATIBABU
1. Usafi wa eneo husika
2. Kutumia nguo za ndan zisizobana na ni vyema kutumia zinazotengemezwa kwa kutumia pamba ili kiruhusu hewa kupita
3. Dawa za kuuwa wadudu lakini pia dawa zenye mchanganyiko wa homoni
4. Kutibu sababu au tatizo husika
5. Upasuaji iwapo uchunguzi utaonesha saratani
By Emmanuel Lwamayanga
Afya ni kitu bora zaidi
.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!