FAHAMU KUHUSIANA NA MALENGE LENGE YATOKANAYO NA MSUGUANO

MALENGELENGE

• • • • • •

FAHAMU KUHUSIANA NA MALENGE LENGE YATOKANAYO NA MSUGUANO


Friction blisters ni malengelenge yanayotokea kwenye ngozi mara baada ya ngozi kujisugua kwenye kitu kingine. Mara nyingi malengelenge haya hutokea kwenye mikono, vidole, miguu na vidole vya miguu.


Tatizo hili huwakumba watoto na watu wazima na mara nyingi huwakumba watu ambao kazi zao uhusisha kutembea au kukimbia kwa muda mrefu kama wanariadha, wapanda milima na wanajeshi.


NAMNA INAVYOTOKEA

malengelenge hutokea baada ya kuwapo kwa msuguano kwenye ngozi. Msuguano huu hupelekea kuvunjikavunjika na kuharibika kwa seli aina ya keratinocytes. Nguvu ya msukumo husababisha maji kukusanyika kwenye sehemu ya ngozi. Nguvu ya msuguano na idadi ya msuguano huamua juu ya kutengenezeka kwa malengelenge. Ngozi yenye unyevunyevu hutengeneza nguvu kubwa ya msuguano ukilinganisha na ngozi kavu. Na mara nyingi malengelenge hutokea sehemu ya ngozi ambayo ni nene na ambayo imejishikiza kwenye sehemu nyingine ya mwili. Katika miguu uvaaji wa viatu vinavyobana ni moja ya sababu.


Magonjwa yanayosababisha ngozi kuwa laini yanachangia mtu kupata tatizo hilo.


DALILI

1. Ngozi kubadilika rangi au kuwa nyekundu

2. Kuhisi maumivu au kuhisi kuchomwa moto katika ngozi.

3. Kutengenezeka kwa malengelenge baada ya masaa kadhaa


MADHARA 

1. Maambukizi katika lengelenge ambayo huepelekea kuongezeka kwa wekundu, maumivu kuwa makali zaidi, na kutoa usaha. 


MATIBABU

kutoboa lengelenge na kupunguza maji yake iwapo litakuwa limeambatana na maumivu. Na baada ya kutobolewa kidonda usafishwa


By Emmanuel Lwamayanga

.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!