FAHAMU KUHUSIANA NA MAUMIVU WAKATI WA HEDHI (DYSMENORRHEA)

HEDHI+MAUMIVU

• • • • • •

FAHAMU KUHUSIANA NA MAUMIVU WAKATI WA HEDHI (DYSMENORRHEA)

 

haya ni maumivu ambayo huambatana na hedhi ambayo humfanya mwanamke ashindwe kufanya kazi zake za kila siku. 


Maumivu haya yamegawanywa katika makundi makuu mawili


A. Maumivu ambayo hutokea pasipokuwa na tatizo kwenye nyonga (via vya uzazi) 

Maelezo, 

Inakadiliwa maumivu makali sana  huwapata asilimia 15-20.  Matumizi  ya vidonge vya majira na dawa za kutuliza maumivu zimepelekea kupungua kwa tatizo hili. 


Sababu za maumivu

Namna ambayo maumivu hutokea haielezeki kwa urahisi lakin huonekana, 

a) huonekana zaidi kwa vijana/mabinti

b) uhusiana na mzunguko wa hedhi

c) maumivu haya upona wakati wa mimba na kuzaa kwa njia ya kawaida

d) inasadikika maumivu haya yanatokana na kujikaza kwa mji wa mimba kusiko na mpangilio. 


1. Uoga na wasiwasi kwa vijana huwafanya waweze kusikia hata maumivu hata kama ni kidogo. 

2. Kufanya kazi kulikopitiliza kwa kuta za mji wa mimba

3. Kuwiana kwa mifumo ya fahamu

4. Prostaglandin 

Kuwako kwa kiwango kikubwa cho homoni ya Progesterone ktk sehemu ya pili ya mzunguko wa hedhi hupelekea kutengenezwa kwa wingi kwa prostaglandin ambazo hupelekea kukaza kwa misuli na hivyo maumivu. 

5. Kuongezeka kwa vasopressin 

6. Endothelins husababisha kujikaza kwa misuli hali inayopelekea kutokufika kwa oksijen na hivyo maumivu


Ni watu gan huwapata? 

Huwapata zaidi mabinti hutokea miaka 2 baada ya kuvunja ungo.  Mama na dada wa binti huyu huweza kuwa tatixo hili. 


DALILI


maumivu huanza masaa machache kabla au huanza wakati hedhi inaanza.  Maumivu haya hudumu kwa masaa kadhaa,  kwa baadhi hufika masaa 24  na nadra hufika masaa 48.


 Maumivu haya huja ghafla hupatikana chini ya kitovu huweza kusambaa kuelekea mgongon na kwenye mapaja,  huambatana na kichefuchefu, kutapika uchovu, kuharisha,  maumivu ya kichwa na mapigo ya moyo kwenda kasi.  Mara chache husababisha mtu kupoteza fahamu. 


MATIBABU 


Iwapo maumivu si makali mtu anahitaji ushauri tu lakin iwapo maumivu ni makali matibabu uhusisha 


1. Dawa 

2. Upasuaji


B.  Maumivu ambayo hutokea ikiwa kuna tatizo kwenye nyonga. 

By Emmanuel Lwamayanga

.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!