MAWE YA KIBOFU
• • • • • •
FAHAMU KUHUSIANA NA MAWE KATIKA KIBOFU CHA MKOJO.
Mawe katika kibofu cha mkojo ni miongoni mwa matatizo yanayowakumba watu wengi. Na hatari za kupata tatizo hili huongezeka zaidi kati ya miaka 40-60. Na huathiri sana wanaume zaidi ya wanawake.
NAMBA AMBAVYO HUTOKEA.
Muundo wa mkojo huamua ni aina gani ya mawe ambayo hutengenezwa. Mawe mengi hutengenezwa na madini au chumvi chumvi na mara nyingi huanza kujikusanya au kuunda mawe iwapo kiwango chake kitakuwa kikubwa kwenye mkojo. Viko vitu/kemikali / madini joto ya mwili ambayo huzuia utengenezaji wa mawe hayo nayo ni
1. Citrate
2. Phosphate
3. Magnesium
NADHARIA ZINAZOONGELEA UTENGENEZWAJI WA MAWE KTK KIBOFU
1. Kutuama kwa damu kwa muda mrefu
2. Maambukizi (bakteria)
3. Kemikali zitokanazo na oksijen nk
4. Dawa.
AINA ZA MAWE HAYA
Aina za mawe katika kibofu inategemeana na aina ya madini yaliyohusika katika utengenezaji nazo ni
1. Mawe yenye calcium
Mawe haya hutengenezwa na aina mbili ya chumvi chumvi za calcium yaani calcium phosphate na calcium oxalate. Na aina hii ndio hupatikana kwa watu wengi. Vihatarishi vyake ni mkojo kuwa na pH isiyo ya kawaida, kuwako kwa kiwango kikubwa cha calcium na oxalate na kuwako kwa kiwango kidogo cha citrate kwenye mkojo.
2. Mawe yenye asidi ya uric
Huweza kutokea kama matokeo ya metaboliki ya purine wakati seli ikivunjwavunjwa lakini pia huweza kutokea iwapo mtu atakula kiwango kikubwa sana cha protini.
3. Mawe aina ya struvite
Kwa majina mengine hufahamika kama magnesium ammonium phosphate na hutengenezwa na baadhi ya bakteria kama p. Mirabilis, k. Pneumoniae na staphylococcus aureus ambao wanatengeneza kenikali iitwayk urease ambayo ubadili urea kuwa ammonia
4. Mawe yenye cystine
Mapungufu/ matatizo ya kimetabolic hupelekea kutokea kwa mawe haina hii.
DALILI
1. Kukojoa mara kwa mara na kuhisi kuwa mkojo umebaki ndani ya kibofu mara baada ya kumaliza kukojoa
2. Maumivu makali mara baada ya kukojoa hasa kwenye kichwa cha uume au mashavu ya uke na mara chache maumivu haya husikika chini ya kitovu. Maumivu haya huchochewa na kutembea na kwa watoto wadogo kitendo cha kupiga kelele na kuvuta uume kwa mkono wakati akimalizia kukojoa ni moja ya dalili.
3. Kukojoa damu
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!