FAHAMU KUHUSIANA NA MICHIRIZI KWENYE NGOZI
MICHIRIZI
• • • • • •
FAHAMU KUHUSIANA NA MICHIRIZI KWENYE NGOZI
Michirizi ni mistari kama makovu ambayo hutokea kwenye ngozi ikiwa na rangi nyekundu au rangi ya kupauka ukilinganisha na sehemu nyingine ya ngozi.
Kuna aina mbili ya hii michirizi
1. Striae rubra hii ni michirizi ya awali ambayo huwa na rangi nyekundu na baada ya muda hubadilika na kuwa
2. Striae alba ambayo hii ni michirizi yenye mpauko wa rangi na hufanania kovu lililosinyaa au kuzoofika.
Michirizi hii hutokea sana kwenye maeneo kama tumboni, kwene matiti, upande wa ndani wa mikono, nyonga, sehemu ya chini ya mgongo, makalio na mapaja.
Japokuwa michirizi haisababishi maumivu, uwepo wake umeambatana na kuharibu muonekano wa ngozi na hata kupelekea gadhabu kisaikolojia.
VIHATRISHI/
1. Mimba/ujauzito
2. Umri (ujana)
3. Dawa mbalimbali
4. Magonjwa
5. Upasuaji
6. Kuongezeka uzito ghafla au kwa haraka
7. Mazoezi ya kujenga misuli
Wakati wa ujauzito imegundulika asilimia kubwa ya wanawake wanaopata michirizi hii wana
1. Historia ya kuwa na mstari ktk mimba zilizopita
2. Uzito mkubwa
3. Kuongezeka uzito sana wakati wa ujauzito
4. Kuwa na mtoto mwenye uzito mkubwa tumboni
5. Kuwa na mimba yenye mapacha wawili au zaidi
6. Kuwa na maji mengi kwenye mfuko wa mtoto
VISABABISHI
Inaaminika kuwa kuongezeka kwa nguvu ya msukumo katika ngozi, mabadiliko ya muundo wa ngozi pamoja na homoni vinachangia utokeaji wa michirizi.
DALILI
mwanzo michirizi hii huonekana kama vimistari vilivyovimba ambavyo hubadiliko kutoka wekundu na kuwa zambarau na kisha huzoofika au kusinyaa na baada ya muda huzinyaa na kutengeneza michirizi kama kovu. Mabadiliko kutoka striae rubra kwenda striae alba huchukua miezi 6-10. Wakati wa ujauzito michirizi huu hutokea kuanzia miezi minne au zaidi na mara nyingi hutokea tumboni, kwenye matiti na kwenye mapaja.
MATIBABU
kwakuwa michirizi hii sio hatari kwa maisha ya binadamu na pia haina ghadhabu basi matibabu yake sio lazima. Matibabu yake uhusisha kuondoa tofauti ya rangi kati ya michirizi na sehemu nyingine za mwili.
Miongoni mwa matibabu ni dawa za kupaka, mionzi, kupandikiza rangi nk. Matibabu hutegemea aina ya michirizi.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!