HEDHI+KUJIFUNGUA
• • • • • •
FAHAMU KUHUSIANA NA MZUNGUKO WA HEDHI MARA BAADA YA KUJIFUNGUA.
Hedhi ya kwanza baada ya kujifungua hutegemea kipindi au zoezi zima la unyonyeshaji. Asilimia 80 ya kina mama iwapo hawatonyonyesha watoto wao, basi hupata hedhi katika wiki ya 12 kutoka siku aliyojifungua. Japo kwa wastani hedhi ya kwanza hutokea wiki ya 7-9 baada ya kujifungua.
Kwa kina mama ambao hawanyonyeshi mayai huanza kupevushwa tangu wiki ya nne na wale wanyonyeshao kupevushwa kwa mayai huanza wiki ya 10 baada ya kujifungua.
NINI KINASABABISHA TOFAUTI HIZI
Idadi ya kunyonyesha kwa siku na muda ambao mtoto ananyonya kwa kila mlo ndio hupelekea tofauti hizo.
Kwa mwanamke anaenyonyesha kiwango cha homoni ya prolactin kwenye damu/mwilini kinakuwa juu hivyo wanawake hao wanakuwa wamelindwa kutokupata ujauzito tena.
JINSI AMBAVYO HOMONI YA PROLACTIN HUFANYA KAZI.
Kiwango kikubwa cha prolactin mwilini huzuia homoni ya kusisimua mayai (FSH) na hali hii hupelekea kutokukuwa kwa yai/ mayai hii hupelekea kiwango kidogo cha homoni ya estrogen kutengenezwa na hivyo mama huyu hatopata hedhi. Lakini pia kiwango hiki kikubwa cha prolactin huzuia kutolewa kwa homoni ambayo hupelekea kupevuka kwa yai (lutenizing hormone) na hivyo yai la mwanamke huyu halitapevushwa. Hivyo kunyonyesha ni moja ya njia za uzazi wa mpango kwa mwanamke aliejifungua
Inashauriwa kwa mama ambaye hanyonyeshi anapaswa kutumia njia za uzazi wa mpango baada ya wiki tatu mara baada ya kujifungua na kwa wale wanyonyeshao wanashauriwa kutumia njia za uzazi wa mpango miezi mitatu baada ya kujifungua.
By Emmanuel
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!