Ticker

6/recent/ticker-posts

FAHAMU KUHUSIANA NA SABABU, DALILI NA MATIBABU YA KUTANUKA/KUKUA/ KUONGEZEKA KWA UKUBWA WA TEZI DUME.



TEZI

• • • • • •

FAHAMU KUHUSIANA NA SABABU,  DALILI NA MATIBABU YA KUTANUKA/KUKUA/ KUONGEZEKA KWA UKUBWA WA TEZI DUME. 


Kutanuka kwa tezi dume imekuwa ni tatizo linalokua sana kwasasa kutokana  na ukweli kwamba muda/umri wa kuishi wa binadamu umeongezeka.  Tezi dume kitaalamu prostate gland hupatikana kwa wanaume na kila mwanaume yupo katika hatari ya kukumbwa na tatizo hili. Ukubwa wa tezi kati ya miaka 20-55 inaaminika kuwa ni gramu 20.


Kutanuka kwa tezi dume kunawapata hasa watu wazima kuanzia miaka 50 na kuendelea. 

Tezi dume imegawanyika katika matabaka/ kanda kuu tatu,  kanda ya pembeni ambayo mara nyingi saratani ya tezi dume hutokea,  kanda ya kati na kanda mpito ambayo huzunguka mrija wa mkojo.  Kanda hii ndio chanzo kikubwa cha tatizo la ukuaji au kutanuka kwa tezi dume. 


KWANINI TEZI INAKUA/INATANUKA. 


Ukuaji wa tezi dume unaendeshwa na visababishi vingi,  kisababishi kikuu ikiwa ni homoni iitwayo testosterone.  Homoni hii hubadilishwa na kuwa homoni ambayo kitaalamu inaitwa DHT ambayo hupatikana kwa wingi katika tezi hii. 


Katika hali ya kawaida kiwango cha testosterone hupungua mwilini kadri umri unavyoongezeka lakini kiwango cha oestrogenic steroids hakipungui kwa uwiano sawa na ule wa testisterone. Hivyo inasadikika kuwa kutanuka kwa tezi dume kunachangikiwa na ongezeko la madhara ya oestrogen. 


Kutanuka kwa tezi dume hupelekea kuongezeka kwa urefu wa mrija wa mkojo. 


DALILI ZA KUTANUKA KWA TEZI DUME


1. mtiririko dhaifu wa mkojo

2. Kukojoa kwa shida,  mkojo kushindwa kutoka hata wakati mtu anapohisi kukojoa

3. Mkojo kuendelea kutoka kidogo kidogo/ matone kwa muda mrefu baada ya kumaliza kukojoa

4. Shida katika kuanza kukojoa au kuubana mkojo

5. Hali ya kujisikia kukojoa mara kwa mara au ghafla

6. Kuhisi kibofu kutokuisha mkojo

7. Kuamka mara nyingi zaidi usiku kwa ajili ya kukojoa

8. Kutumia nguvu kuanzisha mkojo hata pale mgonjwa anapohisi kibofu kimejaa pamoja na maumivu. 


MADHARA 


1. Mkojo kushindwa kutoka kabisa

2. Ukuta na misuli ya kibofu kutanuka na hivyo kupoteza uwezo wa kuzuia mkojo

3. Kuharibika kwa figo

4. Maambukizi ktk njia ya mkojo

5. Mawe katika mfumo wa mkojo. 


MATIBABU 

1. dawa

2. Upasuaji 

Bila kusahau kubadili mfumo wa maisha.






Post a Comment

0 Comments