FAHAMU KUHUSIANA NA SABABU, DALILI, NJIA ZA KUJIKINGA, NA MATIBABU YA MATITI KUJAA NA KUUMA BAADA YA KUJIFUNGUA. (Breast engorgement)

MATITI KUJAA+KUUMA

• • • • • •

FAHAMU KUHUSIANA NA SABABU, DALILI, NJIA ZA KUJIKINGA, NA MATIBABU YA MATITI KUJAA NA KUUMA BAADA YA KUJIFUNGUA. (Breast engorgement)


Miongoni mwa changamoto ambazo huwakumba baadhi ya wanawake katika kipindi baada ya kujifungua ni

1.  Matiti kujaa na kuuma

2. Kupasuka kwa chuchu ama chuchu kuingia ndani na hivyo kuleta changamoto katika kunyonyesha

3. Matiti kuvimba au kutengeneza jipu katika titi

4. Kushindwa kunyonyesha


NINI HUSABABISHA KUJAA KWA MATITI KUNAKOPELEKEA MAUMIVU.


Kujaa kwa mishipa ya damu au mishipa ya lymph kuliko pitiliza kabla ya kuanza kunyonyesha ndio sababu kwanini hali hii hutokea. Kujaa huku huzuia maziwa kutoka.  Wanawake wanaozaa kwa mara ya kwanza ndio mara nyingi hupatwa na changamoto hii.


Mara nyingi hali hii hutokea siku ya 3-4 baada ya kujifungua.


DALILI.

1. Maumivu wakati wa kunyonyesha 2. kuhisi uzito kwenye matiti

3. Kuchoka

4. joto kupanda kiasi


NJIA ZA KUZUIA TATIZO HILI LISITOKEE

1.  Kuepuka matumizi ya vyakula vya awali kwa vichanga (mtoto) kabla hajaanza kunyonya au kabla maziwa hayajaanza kutoka

2. Kuanza kunyonyesha mtoto mapema 

3. Mtoto kunyonya maziwa ya mama tu pasipo kuchanganyiwa chochote.

4. Kuhakikisha mtoto anakaa mkao sahihi kwenye ziwa wakati wa kunyonyesha.


MATIBABU

1. Vaa nguo za kuzuia/kushikilia  matiti (brassiere)

2. Nyonyesha mtoto mara kwa mara.

3. Kamua maziwa iwapo yatabaki mara baada ya kunyonyesha

4. Iwapo maumivu ni makali dawa za kutuliza maumivu hutumika (usitumie bila kushauriwa na mtoa huduma)

5. Muweke mtoto kwenye titi mara kwa mara

6.  Iwapo tatizo ni kubwa sana tumia mashine za kukamlia maziwa.


By Emmanuel Lwamayanga

.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!