FAHAMU KUHUSIANA NA SABABU, MATIBABU NA NJIA ZA KUJIKINGA NA UFA/KUCHANIKA/KUPASUKA KWA CHUCHU (CRACKED NIPPLES).
CHUCHU+KUCHANIKA
• • • • • •
FAHAMU KUHUSIANA NA SABABU, MATIBABU NA NJIA ZA KUJIKINGA NA UFA/KUCHANIKA/KUPASUKA KWA CHUCHU (CRACKED NIPPLES).
Kunyonyesha ni swala linalihitaji ustadi, ujuzi na maarifa. Na iwapo zoezi zima la unyonyeshaji halitofanyika kwa usahihi yapo mambo yanaweza tokea na moja wapo ni hili la kupata ufa katika chuchu la ziwa/titi lako. Ipo mikao sahihi ambayo mama na mtoto wake hupaswa kukaa ili kufanya zoezi zima la kunyonyesha liwe safi na salama kwa wote yaan mama na mtoto.
Tafiti zinaonesha kuwa asilimia 38 ya wanawake wanaonyonyesha hupata tatizo hili na hupelekea zoezi zima la kunyonyesha kuwa gumu.
Ufa katika chuchu huweza kuwapata jinsia zote ila katika makala hii nitaongelea kwa wanawake wanyonyeshao. Kwa wanawake hawa tatizo hili hutokea zaidi ndani ya mwezi wa kwanza baada ya kujifungua. Na hivyo hupelekea baadhi ya wanawake kuacha kunyonyesha mapema zaidi tofauti na inavyotakiwa.
SABABU
Ajari katika chuchu ndio sababu kuu na hii huweza kusababishwa na
1. Mtoto kuwekwa vibaya katika ziwa la mama (kutokuwa na mikao sahihi wakati wa kunyonyesha)
2. Maambukizi katika ziwa
3. Matiti/Ziwa kujaa sana na hivyo kumpa shida mtoto wakati wa kunyonya
4. Nguo zinazobana
5. Kusafisha matiti kwa sababu au kupaka mafuta yenye kemikali.
6. Kutokuwa na ujuzi katika kunyonyesha
7. Kutumia mashine za kukamua maziwa.
MATIBABU
1. kulingana na hali ya tatizo usiendelee kumnyonyesha mtoto kupitia ziwa hilo bali kamua maziwa kisha mnyweshe kwa njia stahiki kisha hiyo chuchu ipakae maziwa yako mpaka yakaukie au paka vaseline katika chuchu hiyo kisha subiri kwa masaa 24-48 ili chuchu ipate kupona.
2. Mama na mtoto mnatakiwa kufata mikao sahihi wakati wa swala zima la kunyonyesha.
3. Usivae bra ambazo zinabana.
NJIA ZA KUZUIA TATIZO
1. osha ziwa lako kwa maji ya uvuguvugu na sio sabuni.
2. Paka mafuta laini yasiyo na kemikali au weka maziwa mpaka yakaukie katka chuchu
3. Mwache mtoto anyonye mpaka aridhike/aache mwenyewe usimkatishe
4. Iwapo maziwa yamejaa sana mpaka kuvimbisha ziwa unaweza ukakamua kiasi kidogo cha maziwa ili kupunguza uvimbe kwan hali hiyo huathiri unyonyaji wa mtoto.
5. Hakikisha mtoto anakaa katika mkao sahihi wakati wa kunyonya.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!